LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 16, 2013

BARAZA KUU LA LAANI VIKALI SHAMBULIO DHIDI YA WALINZI WA AMANI HUKO DARFUR

Na Mwandishi Maalum, New York
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  limelaani vikali shambulio lililofanywa dhidi ya walinda Amani wa Tanzania katika  UNAMID, na limetaka uchunguzi wa kina ufanyike.

Taarifa ya Baraza hilo ambalo ndilo lenye dhamana Kuu ya usimamizi wa Amani ya kimataifa na  jukumu la  kuidhinisha  Misheni zote za ulinzi  wa Amani za Umoja wa Mataifa, imetolewa kwa niaba ya  Baraza  na Marekani ambaye ni Rais wa Baraza hilo kwa mwezi huu wa  Julai.

Taarifa inasema, Wajumbe wa Baraza Kuu la Usalama  wanalaani  kwa nguvu zao   zote mashambulizi yaliyofanyika Julai 13  na  watu wasiojulikana dhidi ya  walinzi wa Amani wa  UNAMID huko Darfur,  waliokuwa katika  doria  katika  eneo la Magharibi ya Nyala Kusini mwa Darfur   na kusababisha vifo vya walinzi  wa Amani  Saba , majeruhi 17, akiwamo  Polisi  huku hali za    majeruhi wawili kati yao ikielezwa kuwa ni  mbaya.

Wajumbe wa Baraza la Usalama Kuu wanatoa salamu zao za rambirambi kwa familia za walinzi hao wa Amani waliopoteza  maisha katika shambuli hilo, na pia  kwa Serikali ya Tanzania na kwa  UNAMID.

Baraza Kuu  la Usalama  limeitaka Serikali ya Sudan kufanya uchunguzi wa kina  juu na tukio hilo na kuwafikisha  mbele ya mkono wa sheria wale wote waliohusika.

Taarifa hiyo inaeleza zaidi kwamba. Baraza Kuu la Usalama ,  limeonyesha  wasiwasi wake  kuhusu mazingira ya shambulio hilo, moja ya   shambulio baya  kuwahi   kufanyika  dhidi ya walinzi wa UNAMID tangu kuanzishwa kwake.

Baraza Kuu la Usalama katika taarifa yake hiyo limesisitiza kwamba shambulio au vitisho vya aina yoyote dhidi ya  UNAMID havikubaliki. Na limetaka kutojirudia tena kwa  tukio kama hilo.

Vile vile Baraza Kuu la Usalama  limerejea  msimamo wake  kwamba linaunga mkono kwa kauli moja Misheni ya kulinda Amani ya UNAMID na  limetoa wito kwa pande zote huko Darfur  kushirikiana na   Misheni hiyo.

Wakati huo huo, kufuatia tukio hilo la kusikitisha, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa  Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi, amekuwa akipokea kwa niaba ya serikali na familia, salamu za pole   kutoka kwa Mabalozi wenzake.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages