Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sekretarieti ,Makao Makuu ya CCM ,Dodoma leo tarehe 13/2/2013. |
TAMKO LA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA
CCM KUHUSU MAANDAMANO NA VURUGU ZILIZOTOKEA MKOANI MTWARA JUU YA UJENZI WA
BOMBA LA GESI
NA MAENDELEO YA MKOA WA MTWARA
1. Halmashauri
Kuu ya Taifa imepokea maelezo ya Serikali kuhusu maandamano na vurugu zilizotokea
Mkoani Mtwara tarehe 27 Desemba, 2012 tarehe 25 Januari, 2013 na tarehe 26
Januari, 2013. Maandamano na vurugu hizo zilizodaiwa kuwa na lengo la kupinga
mradi wa bomba la Gesi kujengwa na kupeleka Gesi Dar es Salaam .
2. Baada ya kupokea maelezo haya ya
Serikali, Halmashauri Kuu ya Taifa imebaini kuwa: -
(a)
Kwa
sehemu kubwa Wananchi wa Mkoa wa Mtwara hawakuwa wamepewa elimu ya kutosha juu
ya uendelezaji wa Gesi na jinsi watakavyonufaika.
(b)
Baadhi
ya Wanasiasa na baadhi ya Viongozi wa Makundi mbalimbali waliamua kutomia suala
la Gesi kupandikiza lugha za chuki, uchochezi na upotoshaji wa maendeleo ya
Mradi wa Gesi kwa lengo la kujitafutia umaarufu.
(c)
Suala
la Gesi limetumika kama kisingizio tu cha
kufanya vitendo vya rurugu na uvunjifu wa amani.
3. Kutokana
na ukweli huu, Halmashauri Kuu ya Taifa inaelekeza ifuatavyo:-
(i)
Imesikitishwa
na vurugu zilizotokea na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha na uharibifu
mkubwa wa mali na majengo ya CCM, Serikali, Wabunge na watu binafsi.
Halmashauri Kuu ya Taifa inawapa pole wafiwa na waliopoteza mali zao.
(ii) Inaiagiza
Serikali kufanya uchunguzi wa kina kuhusu waliofanya vurugu na uharibifu
mbalimbali na kuwachukulia hatua kwa mujibu wa Sheria. Pia, kuwa makini na
kuhakikisha matukio kama haya hayajitokezi
tena.
(iii)
Inaiagiza
Serikali kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwa Wananchi wa maeneo husika kuhusishwa na kuelimishwa juu ya miradi
mbalimbali kwenye maeneo yao .
(iv)
Halmashauri
Kuu ya Taifa inawataka Wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuendelea kuishi kwa amani na
utulivu kama ilivyo desturi yao, maana vurugu pamoja na kuharibu mali na
kugharimu maisha vinaweza kuwakimbiza
wawekezaji waliojitokeza na ambao
shughuli zao zitawafaidisha
wananchi wa Mkoa huu na Watanzania kwa ujumla .
HALMASHAURI KUU YA TAIFA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇