Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, ukiingiwa kwenye eneo la Uwanja wa Ndege wa Kigoma uliopo eneo la Kipampa, kwa ajili ya kushuhudia maendeleo yaliyofikiwa katika ujenzi mkubwa wa kiwanja hicho unaoendelea ili kukiongezea uwezo.
Mafundi wa kampuni ya Resident Engineer inayokarabati uwanja huo wakiwa kazini wakati msafara wa Kinana unakagua uwanja huo leo jioni
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwasalimia wafanyakazi kwenye uwanja huo alipowasili.
Meneja wa Uwanja huo, Elipind Tesha (kulia) akimweleza Kinana na ujumbe wake hatua ilipofikiwa katika ujenzi huu, ambapo alisema, umefikia asilimia tisini, na kwamba unaweza ingawa unaweza kuanza kutumika rasmi Aprili mwaka huu, lakini matengenezo yote yatakuwa yamekamilika Juni 2013. Wengine kutoka kushgoto ni, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martin Shigela.
Kazi ya kupanua Uwanja ikiendelea
Msafara wa Kinana ukipita kwenye eneo la matengenezo makubwa yanayofanyika kwenye Uwanja huo.
Nape akijaribu kuendesha moja ya vijiko vinavyotumika kufanya kazi kwenye ujenzi huo. Alibeba mapipa ya lami kwa kutumia kijiko hicho na kukiendesha kuyatoka eneo moja kwenda lingine.
Kinana akimsikilliza Mhandisi Mkazi wa Uwanja huo,Cleopa Mpembeni (wapili kulia) akimpa maelezo ya kiufundi kuhusu ujenzi unavyoendelea.
Msafara ukitoka baada ya ukaguzi huo. Ambapo Kinana akizungumza amewataka wananchi wa Kigoma na Watanzania kwa jumla kuzitumia fursa za kibiashara zitakazopatikana kutokana na kuboreshwa kwa Uwanja huo. (Picha zote na Bashir Nkoromo).
Your Ad Spot
Jan 28, 2013
Home
Unlabelled
KINANA NA MSAFARA WAKE WAKAGUA MATENGENEZO YA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA
KINANA NA MSAFARA WAKE WAKAGUA MATENGENEZO YA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇