Kampuni ya Lakeland Africa ya jiji Dar es Salaam imeandaa
safari ya kutembelea hifadhi za taifa na makumbusho ya taifa ili kutoa fursa
kwa Watanzania kusherehekea msimu huu wa Krismas na Mwaka mpya.
Watanzania wanahamasishwa
kujitokeza kushiriki katika safari hiyo ya kitalii ya siku 14 itakayoanza
jumamosi ya Desemba 14 mwaka huu hadi Desemba 27 mwaka huu. “Kwako mtanzania
sasa inawezekana kujua Tanzania yako, si lazima kuwa mzungu kuwa mtalii wa
ndani”
Safari hii itaanzia Dar es Salaam, na kupita katika hifadhi
za Sadan, Pangani, Lushoto, Tarangire, Ziwa Manyara, Ngorongoro Crater, Hifadhi
ya Serengeti na itahitimishwa Butiama kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Safari hii itatumia magari ya kisasa makubwa yenye uwezo wa
kubebe watalii 24 na kutoa nafasi kutumia vifaa vya umeme (laptop, simu, kamera)
kwa kila mtalii kuwa na soketi yake. Magari ambayo yamekuwa yakitumiwa na
makampuni ya utalii katika nchi za ulaya sasa kutumika Tanzania pia.
Gharama za safari hii zinajumuisha chakula, malazi, usafiri,
tozo za kuingia hifadhini na tiketi ya ndege kutoka Mwanza kurudi Nyumbani.
Kwa mawasiliano na Lakeland Africa
‘Kuwa mtalii ndani ya nchi yako’
naipongeza kampuni hii ya kizalendo kuhamasisha utalii wa ndani. hivi vivutio ni nyetu ni aibu ikiwa asilimia kubwa ya Watanzania tukawa hatujavitembelea. Tutumie hii fursa nzuri kutembelea vivutio vyetu kwa gharama nafuu
ReplyDelete