Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akimjulia hali Padri Ambros Mkenda wa
Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya
mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo
Jumamosi Desemba 29, 2012 kufuatia kupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu
wasiojulikana mapema wiki hii wakati akisubiri kufunguliwa geti la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini
Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais
Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka. |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇