LINDI TANZANIA
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amezindua Mahakama ya Mwanzo katika Eneo la Londo Mnara Wilaya ya Lindi Vijijini Mkoani Lindi. Mheshimiwa Rais ameambatana na Waziri wa mambo ya nje ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani humo Mheshimiwa Bernard K. Membe.
Katika Hotuba yake ya Ufunguzi Mheshimiwa Rais aliwataka wananchi wa Londo kufuata utaratibu wa sheria katika kuwashughulikia waarifu wa makosa mbalimbali na kuchukua sheria mikononi. Mheshimiwa Rais pia alieleza katika hotuba yake hiyo kuwa mahakama ni muhimili mkubwa wa Serikali na hivyo ni vizuri ikitumika ipasavyo na kutoa haki kwa kila mtu.
Pia alimuita Diwani wa Eneo hilo na kumuuliza juu ya Changamoto na Kero za Eneo hilo na Diwani alitaja kuwa kero kubwa ni tatizo la Maji, barabara pamoja na kutokuwepo kwa Kituo cha Polisi, ambapo Mheshimiwa Rais alichangia shilingi milioni tatu 3000,000 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha polisi na pia kumuagiza Mkurugenzi alete mabomba ya maji haraka katika Eneo hilo na pia akawahimiza makandarasi wa barabara kujitahidi kukamilisha Ujenzi huo haraka iwezekanavyo.
Mheshimiwa Rais yupo katika ziara ya siku tano Mkoani Lindi ambapo leo join atahutubia katika wilaya ya Ruangwa na Nachingwea.
hongera mheshimiwa Raisi kwa ufunguzi wa mahakama hiyo ya rufaa pamoja na uchangiaji wa ujenzi wa kituo cha polisi, mambo hayo kwa pamoja yatasaidia usimamiaji wa sheria na haki! kidumu chama cha mapinduzi
ReplyDeletehongera mheshimiwa Raisi kwa ufunguzi wa mahakama hiyo ya rufaa pamoja na uchangiaji wa ujenzi wa kituo cha polisi, mambo hayo kwa pamoja yatasaidia usimamiaji wa sheria na haki! kidumu chama cha mapinduzi

ReplyDelete