RAIS Jakaya Kikwete amesema serikali
ina mpango wa kujenga uwanja wa ndege wa
kimataifa katika mji wa Mugumu, wilayani Serengeti, ili kurahisisha usafiri kwa
watalii waendao au kutoka kwenye vivutio vya utalii vilivyopo kanda ya
kaskazini.
Amesema hayo mbele ya wajumbe wa
Mkutano Mkuu wa 8 wa CCM unaoendelea mjini Dodoma.
Kauli hiyo ya mwenyekiti wa ccm
ameitoa alipokuwa akifafanua kuhusu taarifa iliyosomwa na Naibu Waziri wa
Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba, mbele ya wajumbe hao kuwa serikali itajenga
kiwanja hicho.
Akitoa ufafanuzi huo, Rais Kikwete
amewaeleza wajumbe hao kwamba uwanja utakaojengwa utakuwa eneo la Mugumu na sio
kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Amesema kuwa hatua hiyo ya ujenzi wa
kiwanja hicho cha ndege utawawezesha watalii uchaguzi wa ama kutua Mugumu
au Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro.
Amesema kwa watalii watakaoshukia
uwanja wa KIA na kutembelea hifadhi ya Tarangire, Manyara, Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongoro (NCAA) wataweza kuondoka kurejea makwao kwa kutumia uwanja
utakaojengwa Mugumu badala ya kurudi tena hadi KIA.
Hali kadhalika amesema, watalii
watakaoshuka kwenye uwanja utakaojengwa Mugumu hawatakuwa nahaja ya kurudi tena
Serengeti ili warejee makwao kwa kuwa wataendelea kutembelea vivutio vingine
kwenye katika Hifadhi za Manyara, Tarangire, Anapa hadi Mlima wa Kilimanjaro na
kurejea makwao kwa kutumia uwanja wa KIA.
Akizungumzia kuhusu Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Songwe, dk kikwete amesema umekwishakamilika na uzinduzi wake
unatarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu.
Amesema uwanja huo uko kusini na
yapo mashirika kadhaa ya ndege ya kimataifa ambayo yameomba ndege zao ziwe
zinatua kwenye uwanja huo wakati zikifanya safari zake za kwenda nchi za Kusini
mwa Afrika.
Aidha amesema upo mpango kabambe wa
kulitumia eneo la ukanda wa Nyanda za Juu Kusini kwa kilimo kikubwa cha maua
ambayo yatakuwa yakisafirishwa kwenda kuuzwa nje kupitia uwanja huo.
Ametanabaisha kuwa kwa sasa serikali
itaelekeza nguvu zake katika kuhakikisha kanda ya Nyanda za Juu Kusini, inapewa
msukumo kwa kilimo kikubwa cha maua
ambacho tutakipa nguvu zaidi ili yasafirishwe kwenda kwenye masoko ya nje.
RAIS Jakaya Kikwete amesema baada ya
kupatikana kwa gesi asilia kiasi cha mita za ujazo trilioni 33 , serikali kwa
kuanzia inatarajia kujenga gridi ya taifa ya gesi jijini Dar es Salaam, kwa
ajili ya matumizi ya viwandani na majumbani.
Amesema gesi itakayopatikana
itatumika kwa matumizi ya viwandani na majumbani na kiasi kingine kitauzwa nje.
Amesema baada ya kukamilika giridi
ya gesi, wakazi wa Dar es Salaam watakaohitaji kupata gesi hiyo kwa matumizi ya
majumbani kwao watapelekewa.amesema utaratibu kama huo utafanyika kwa mikoa
mingine.
Amesema upatikanaji wa gesi hiyo
utaifanya Tanzania iweze kukuza uchumi wake kwa kuwa itatumika kwa uzalishaji
wa bidhaa viwandani, mbolea na uzalishaji wa umeme.
Hata hivyo, amesema gesi itayouzwa
nje itasafirishwa kwa kupitia bandari za Mtwara na Kilwa kwa kuwa itakuwa
gharama kuisafirisha hadi Dar es Salaam katika lengo la kuiuza nje.
Amesema sera ya gesi inatarajiwa
kukamilika hivi karibuni pamoja na kuweka miundombinu itakayowezesha kudhibiti
uhujumu wa biashara hiyo nje ya nchi.
Nimeshtuswa sana na habari hii niliposikia serikali ina mpango wa kujenga kiwanja cha ndege nje ya hifadhi ya Serengeti.ninacho jiuliza ni kuwa nchi nyingi hua wanataka na wanawakaribish watalii kukaa ndani ya nchi kwa mud a mwingine iwezekanavyo ili kupata mapato zaidi na kulinda ajira za wananchi wao.sasa kwa kite do hichi cha kujenga hicho kiwanja huko ni kumaanisha hatuwataki Hawa watu ? Na kuzingatia kua kiwanja cha KIA na arusha hakina umbali wa hivyo wa kusema inakua karaha kwa wageni wetu.
ReplyDeleteNi jambo la kushangaza sana kutaka watalii waondoke haraka haraka ili iwe nini ? Wanapotoka nyie ngorongoro kwa kawaida wanasimama Arusha au moshi kwa mapumziko ya siku moja AMA mbili kabla ya kuendelea na safiri ya kurudi makwao na katika muda huo wenzetu wa mahoteli restaurants na hata wauza vinyago hufaidika na watalii hawa.
Rais wetu ni Mtu wa busara sana namini lakini kwa hili sikutegemea au labda ushauri alopewa sio mzuri .
Naomba niwakilishe maoni yangu.