LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 18, 2012

MKUTANO WA MAPOKEZI YA MWENYEKITI NA SEKRETARIETI MPYA YA CHAMA CHA MAPINDUZI.

DAR ES SALAAM, TANZANIA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya mnazi mmoja, ambapo yamefanyika mapokezi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Sekretarieti Mpya iliyoundwa baada ya Mkutano Mkuu wa Chama uliofanyika hivi karibuni katika Mji wa Dodoma.

Mkutano huo mahsusi kwa mkoa wa Dar es Salaam kufanya sherehe za mapokezi ya viongozi wapya waliochaguliwa na kupitishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi kuwa safu mpya ya kukisimamia, kukiimarisha na kukiendeleza Chama..

Mkutano huo ambao ulianza majira ya mchana wa saa nane na kumalizika saa kumi na mbili ulitawaliwa na matukio mbalimbali zikiwemo hotuba muhimu kutoka kwa viongozi hao wapya ambao walisisitiza kuwa sasa kikosi kamili kimetimia na yale ambayo yalikuwa yanawakwaza wanaCCM likiwemo suala la Rushwa katika chaguzi, upendeleo na kupanga safu ya uongozi kwa maslahi binafsi, Katibu Mkuu wa Chama Hicho alisisitiza juu ya Kuondoa kabisa tatizo la UBINAFSI ambalo ndio chanzo kikubwa cha makundi na migogoro katika chama hicho.

*ZIAFUATAZO NI PICHA ZA BAADHI YA MATUKIO YALIYOSISIMUA
Melfu wakiwa wamefurika katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam, wakati wa mapokezi rasmi ya Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Rais Jakaya Kikwete na safu yote mpya ya uongozi wa CCM. (picha na Bashir Nkoromo)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia baadhi ya viongozi
 Mmoja wa wanan-CCM waliohudhuria sherehe hizo, akiwa na bango kufikisha ujumbe wa wengi
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na meza kuu wakiwa wamesimama wakati ukiimbwa wimbo maalum wa CCM wakati wa sherehe hizo
 Asley na Tundaman wakitoa burudani kwenye mkutano huo
 Mapema Rais Kikwete alikabidhiwa shada la maua  na mtoto maalu
 Mama Salma Kikwete ambaye pia alikuwepo mstari wa mbele katika sherehe hizo, alikabidhiwa shada la maua
Ikawa ni kujimwaya mwaya hadi mwisho wa sherehe, Picha zote na Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages