Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari,ofisi ndogo za CCM Lumumba,Dar es salaam. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUTANO MKUU WA CCM 2012
Kikao
cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kilichofanyika tarehe 13/10/2012
pamoja na mambo mengine kilipanga ratiba ya Mkutano Mkuu wa Taifa iwe kama ifuatavyo:-
1.
Mkutano
Mkuu wa Nane wa Kawaida wa CCM utafanyika tarehe 10 – 12 Novemba, 2012 . Kwa kawaida Mikutano Mikuu ya CCM imekuwa
ikifanyika kwa siku mbili. Lakini safari
hii CCM imeamua mkutano huo uwe wa siku tatu ili kutoa fursa kwa Wajumbe
kujadili kwa kina taarifa muhimu zitakazowasilishwa.
2.
Mkutano
huo utafanyikia KIZOTA – Dodoma
mahali ulipofanyika Mkutano Mkuu uliopita mwaka 2010.
3.
Shughuli
muhimu zitakazofanywa wakati wa Mkutano huo zitakuwa:-
(1)
Kufanya
marekebisho ya Katiba ya CCM ya 1977 toleo la 2010 kwa kuzingatia mapendekezo
ya Halmashauri Kuu ya Taifa yatakayowasilishwa kwenye Mkutano huo.
(2)
Kupokea
na kujadili taarifa mbalimbali zikihusu:-
(i)
Taarifa
ya Kazi za Chama kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2007-2012
itakayowasilishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.
(ii)
Taarifa
ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ya Serikali ya Jamhuri
ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .
4.
Shughuli
za Uchaguzi ambazo zitahusu Uchaguzi wa:-
(i)
Wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa Viti Kumi vya Bara na kumi vya Zanzibar .
(ii)
Mwenyekiti
wa CCM.
(iii)
Makamu
wawili wa Mwenyekiti mmoja kutoka Bara na mwingine kutoka Zanzibar .
Shughuli za Mkutano Mkuu zitatanguliwa na
kuweka Jiwe la Msingi la Majengo ya Ukumbi wa Mikutano na Makao Makuu ya CCM
eneo la Medelii katika Manispaa ya Dodoma . Shughuli hii itafanywa na Mwenyekiti wa CCM
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
MAANDALIZI
YA MKUTANO
Shughuli za Maandalizi ya Mkutano
zinaendelea vizuri. Shughuli hizi ni
pamoja na uchapaji wa Nyaraka mbalimbali; usafiri wa Wajumbe, Maandalizi ya
Ukumbi na huduma nyingine muhimu kwa ajili ya kufanikisha Mkutano huo.
VURUGU
ZILIZOTOKEA MBAGALA
Chama cha Mapinduzi kimesikitishwa na
matukio yaliyotokea Mbagala, jijini Dar
es Salaam , tarehe 11 Oktoba 2012. Chama Cha Mapinduzi
kinalaani kitendo cha kukojolewa kwa kitabu kitakatifu cha dini ya Kiislam,
yaani Kuran. Vilevile, Chama cha Mapinduzi kinalaani vitendo vya vurugu na
kuvamiwa na kuchomwa moto makanisa.
Vitendo vyote hivi havifanani na mila na
desturi za Watanzania. Kitendo cha kukojolea kitabu kitakatifu cha Waislamu
hakikubaliki. Na kitendo cha kuvamia na kuchoma moto nyumba za ibada za
Wakristo na kufanya vurugu pia hakikubaliki. Tanzania ni nchi inayofahamika na
kusifika kwa amani na utulivu na kwa umoja na mshikamano wa watu wake wa kabila,
rangi na dini zote. Chama Cha Mapinduzi kinawasihi wananchi wawe na subira na
uvumilivu yanapotokea matukio kama haya na
waviachie vyombo vya dola vifanye kazi yake.
Ni imani ya CCM kwamba vyombo vya dola
vitachukua hatua stahiki kwa wote waliohusika na matukio haya. Pia, tunatumaini
kwamba hali ya amani na utulivu itarejea Mbagala kama
kawaida.
UTEUZI WA MAJINA YA
WAGOMBEA NAFASI MBALIMBALI
MKOANI KILIMANJARO
Kamati Kuu pia imefanya uteuzi wa mwisho wa
majina ya Wanachama wa CCM walioomba nafasi za Uongozi ndani ya Chama Cha
Mapinduzi katika nafasi za Uenyekiti wa CCM Wilaya na Ujumbe wa Halmashauri Kuu
ya Taifa nafasi ya Wilaya za Siha na Moshi Vijijini.
Kwa mujibu wa Katiba ya CCM; uteuzi wa
mwisho wa nafasi hizi hufanywa na Halmashauri Kuu ya Taifa, lakini Kikao cha
tarehe 25/9/2012 kilichofanyika Mjini Dodoma hakikufanya uteuzi wa wagombea wa
nafasi hizi katika Wilaya za Siha na Moshi Vijijini. Hivyo, Kikao hicho
kilikasimu madaraka yake ya uteuzi kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Nafasi za Uongozi zinazogombewa na majina ya
walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-
(1) Nafasi
ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Moshi
Vijijini
Waliojitokeza
kugombea nafasi hii ni 13. Walioteuliwa
ni wanne (4) wafuatao:-
(a) Ndugu
Shayo Isack EDWARD
(b) Ndugu
Masenga John GABRIEL
(c) Ndugu
Shao C. GEOFREY
(d) Ndugu
Mallya Mathew MARTIN
(2) Nafasi
ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Siha
Waliojitokeza
kugombea nafasi hii ni wanne (4).
Walioteuliwa ni wanne (4) wafuatao:-
(a) Ndugu
Tawida Nahato BASSO
(b) Ndugu
Simon Lekshon MOLLEL
(c) Ndugu
Happiness Mathias MUNUO
(d) Ndugu
Oscar Jeremiah TEMI
(3) Nafasi
ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa Wilaya ya Siha
Waliojitokeza
kugombea nafasi hii ni saba (7).
Walioteuliwa ni wanne (4) wafuatao:-
(a) Ndugu
Meijo Loloinyo LAIZER
(b) Ndugu
Joha Shabani MTAWAZO
(c) Ndugu
Happiness Mathias MUNUO
(d) Ndugu
Cosmas Sebastian MUSHI
Imetolewa
na:
Nape Moses Nnauye,
KATIBU
WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
IDARA
YA ITIKADI NA UENEZI
14/10/2012
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇