LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 11, 2012

TANZANIA YAUKWAA TENA UJUMBE BARAZA LA UTAWALA LA UMOJA WA POSTA DUNIANI

NA INNOCENT MUNGY DOHA, QATAR
Tanzania imechaguliwa tena kuingia katika Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani (UPU), kipindi kingine cha miaka minne baada ya kuwa miongoni mwa nchi 40 kati ya nchi 192 wanachama wa umoja huo.

Katika uchaguzi wenye ushindani mkubwa na diplomasia ya hali ya juu, nchi nyingi zilikusudia kuingia kwenye Baraza hilo. Tanzania imekuwa moja ya nchi mbili za Afrika Mashariki, ikiwamo Uganda kushinda nafasi hizo. Nchi nyingi e za Africa zilizofanikiwa kuingia katika Baraza hilo ni Burkinafaso, Jamhuri ya Congo Brazaville, Ivory Coast, Misri, Gabon, Malawi, Morocco, Sudan na South Africa.

Mapema leo asubuhi, Balozi Hussein A. Bishar wa Kenya alichaguliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa UPU akimshinda mwanamama Serrana Casco kutoka Uruguy. Nafasi ya Naibu Mkurugenzi Mkuu iliyokuwa na ushindani mkubwa kati ya Mmarekani Denis Delehantty na Mswiss Pascal-Thienry Clivaz ambapo Clivaz alishinda nafasi hiyo.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh. Prof. Makame Mbarawa wakifurahia ushindi wa Tanzania kuchaguliwa katika Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani leo. Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi 40 zinazounda Baraza hilo, Kati ya nchi wanachama 192

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages