LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 4, 2012

VIONGOZI WA {TROIKA} YA SADC WAKUSANYIKA DAR ES SALAAM KWA MKUTANO.

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) akimpokea  Rais Armando Guebuza wa Msumbiji baada ya kuwasili Septemba 3, 2012 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, tayari kwa mkutano wa Troika ya SADC unaotarajiwa kufanyika Septemba 4, 2012 katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency na kuhudhuriwa na viongozi wa nchi wajumbe wa Asasi hiyo ambao ni Msumbiji ambao ni Mwenyekiti wa sasa wa SADC, Afrika Kusini aliyekuwa Mwenyekiti wa Asasi hiyo kabla ya Tanzania,  Namibia ambao ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi hiyo ya Troika, pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambao ni wageni waalikwa.

 Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (Troika) ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) akimuonesha   Rais Armando Guebuza wa Msumbiji mandhari ya Bandari ya Dar es salaam kutoka  katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages