Wabunge saba wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii ya Bunge la Jamhuri ya Muungano pamoja na
Wajumbe wawili wa Baraza la Wawakilishi mmoja kutoka Kamati ya Mifugo, utalii, uwezeshaji na Habari na mwingine kutoka Kamati ya katiba na Sheria wanaenda India Septemba 23 kwa siara ya siku tano.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) , Kajubi Mukajanga amesema Baraza limeandaa ziara hiyo kwa lengo la kuwapa fursa Wabunge na Wawakilishi kupata ufahamu wa nchi inayoendelea yenye sheria ya Haki ya Kupata Habari.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari katika ofisi za MCT, Mukajanga alisema ziara hiyo imo katika mpango kazi wa mwaka huu wa Baraza la Habari kupeleka kundi la Wabunge na Wawakilishi katika nchi moja inayoendelea ambayo ina sheria ya Haki ya Kupata Habari.
Sababu ya kuchagua nchi inayoendelea ni kuhakikisha kuwa Wabunge na Wawakilishi wanapata uzoefu katika nchi yenye mazingira na hali inayofanana na nchi yetu, amesema.
Mukajanga amesema kwamba uzoefu wa Baraza la Habari kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano hivi katika mchakato wa kupata sheria ya Haki ya Kupata Habari umeonyesha kuwa kuna wasiwasi kuhusu sheria hiyo kwamba inaweza kuleta vurugu ama fujo.
Baraza la Habari, alisema Mukajanga, linataka wabunge ambao ni watunga sheria, waende wakajifunze, wakaulize maswali na waelewe umuhimu wa kuwa sheria hiyo.
Aliongeza kuwa ziara hii ya mafunzo kwa Wabunge na Wawakilishi imeandaliwa na MCT kwa mtazamo kwamba “kuona ni kuamini”.
Msafara huo wa wabunge na wawakilishi utaongozwa na Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mheshimiwa Juma Nkamia.
Wabunge wengine katika msafara huo ni: Rebecca Michael Mngodo, Ramadhani Haji Saleh, Hussein Mussa Mzee, Assumpter Nshunju Mshama, Moza Abeid Saidy na Said Mtanda . Wawakilishi ni Ali Mzee Ali na Ismail Jussa Ladhu.
Akizungumza katika mkutano huo, kiongozi wa msafara huo, Nkamia aliipongeza MCT kwa kuona umuhimu wa kuwaandalia wabunge ziara hiyo ya mafunzo nchini India.
Alisema watatumia watakayojifunza katika ziara hiyo kufanikisha upatikanaji wa sheria ya haki ya kupata habari nchini.
Wabunge wote waliomo kwenye msafara huo walieleza kwenye mkutano huo kuwa bila shaka watanufaika na safari hiyo ya mafunzo na watatumia uzoefu watakaoupata kufanikisha kupitishwa sheria ya haki ya kupata habari.
Wabunge na Wawakilishi hao watafuatana na maofisa watatu wa Baraza la Habari ambapo wawili John Nguya na Ziada Kilobo wanatoka Dar es Salaam na mmoja, Shifaa Hassan anatoka Zanzibar.
Miongoni mwa sehemu watakazotembelea Wabunge na Wawakilishi ni pamoja na Ubalozi wa Tanzania mjini New Delhi, Ofisi ya Tume Kuu ya Habari, Ofisi ya Tume ya Habari ya Jimbo, Kituo Kikuu cha Habari cha Umma, Idara ya Utumishi na Mafunzo na Ofisi ya Taifa ya Kampeni ya Haki ya Kupata Habari.
Akijibu swali kuhusu kwanini wanahabari hawakujumuishwa kwenye msafara huo, Mukajanga alisema kuwa Baraza litawaandalia ziara kama hiyo wanahaabari mwakani.
Alifafanua baadaye kuwa ziara hiyo inaweza kuwa India ama Afrika Kusini.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇