Katibu wa Halmashauri Kuu Taifa-Itikadi na Uenezi, Mh. Nape Nnauye akisalimiana na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wa wilaya ya Mpanda, mkoa wa Katavi.
Viongozi wakuu wa Chama cha Mapinduzi wakishiriki maandamano kuelekea kwenye uwanja wa Kashaulili wilaya ya Mpanda.
Wapenzi na wanachama wa CCM wa Mkoa wa Katavi wakiwaongoza viongozi wa chama na serikali kwenye uwanja wa Kashaulili wilaya ya Mpanda ambapo viongozi hawa watahutubia na kuambia wananchi utekelezaji wa ilani ya CCM.
Mh.Nape akihutubia wananchi wa Mpanda waliofurika kwenye uwanja wa Kashaulili,ambapo alikemea vikali vitendo vya vyama vingine kuendekeza vurugu badala ya siasa.
Mh.Mwigulu Mchemba akieleza wananchi masuala muhimu ya kiuchumi na kwa nini kunakuwa na mfumuko wa bei,pia alitumia fursa hiyo kukemea mauaji yalotokea kwenye jimbo lake ambapo kijana mmoja kiongozi wa chama aliuawa na wanachama wa chama cha upinzani.
Waziri wa Maji Prof.Jumanne Maghembe akihutubia wananchi wa Mkoa wa Katavi, ambapo ameahidi kulitatua tatizo la maji haraka iwezekanavyo na pia kutoa tamko la kushushwa kwa bei za maji.
Naibu Waziri Wizara ya Uchukuzi,Mh. Charles Tizeba akizungumzia masuala ya kuimarisha reli na pia utunzaji wa treni zetu ikiwa suala zima la usafi, pia aliwaambia wananchi serikali imeagiza mabehewa ya abiria na ya mizigo.
Naibu Waziri Kilimo na chakula,Mh. Adam Malima akihutubia wananchi wa mkoa wa Katavi, juu ya masuala mabali mbali ambayo yametekelezeka likiwemo suala la umeme na pia aliwaambia wakulima kwamba serikali imeandaa utaratibu mzuri wa vocha za kilimo ambazo utatangazwa hivi karibuni.
Your Ad Spot
Jul 16, 2012
Home
Unlabelled
VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI WAHUTUBIA WANANCHI WA KATAVI LEO
VIONGOZI WA CHAMA NA SERIKALI WAHUTUBIA WANANCHI WA KATAVI LEO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇