NA BASHIR NKOROMO, DAR
Jakaya Kikwete amesema serikali haitawalipa madaktari mishahara ya sh. milioni 3.5 wanayoshinikiza kupata na badala yake imewataka wasiokubali kuendelea na kazi waondoke.
Jakaya Kikwete amesema serikali haitawalipa madaktari mishahara ya sh. milioni 3.5 wanayoshinikiza kupata na badala yake imewataka wasiokubali kuendelea na kazi waondoke.
Katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi Juni, aliyoitoa jana, Rais Kikwete amesema serikali haina uwezo wa kulipa kiasi hicho kwa kuwa uwezo wake ni mdogo.
“Kutokana na ukweli huo basi kama kuna daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi serikalini bila kulipwa mshahara huo, awe huru kuacha kazi na kwenda kwa mwajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo,” alisisitiza. HOTUBA KAMILI YA RAIS BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇