LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 5, 2012

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WABUNGE WA TANZANIA KATIKA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza  na Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukutana nao Juni 4, 2012 katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha.Wabunge hao wapo Arusha tayari kwa kikao chao cha kwanza na wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi Leo ambapo wanatarajiwa kuchagua Spika wa Bunge hilo pamoja na kuapishwa tayari kuanza majukumu yao.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt  Jakaya Mrisho kikwete,  jana Juni 4, 2012 amekutana na Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.
Mhe. Rais, ambaye aliwakaribisha Wabunge hao kwa chakula cha mchana katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge, aliwapongeza kwa kuchaguliwa kwao kuiwakilisha Tanzania katika Bunge hilo la Jumuiya, na kuwataka wasimamie na kutetea maslahi ya nchi wakiwa huko.

Pia Rais amewataka Wabunge hao kuwa karibu na Serikali katika kushauriana namna ya kukabiliana na changamoto zitazojitokeza katika kazi zao, na kuwakumbusha kwamba majukumu ya Bunge hilo la Jumuiya ni kusimamia makubaliano  (treaty) yaliyoorodheshwa  katika kuundwa kwake na kuendeshwa.

Alisema: “Msome vyema na kuyaelewa makubaliano (treaty) hayo yote na vipengele vyake na msaidie kuiendeleza Jumuiya ambayo wanachama wote watanufaika nayo, na siyo upande mmoja.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages