Mbunge wa Korogwe Vijijini(CCM) Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu", akizungumza na waandishi habari. Mbunge wa Korogwe Vijijini(CCM), Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu", akizungumza na waandishi habari mjini Dodoma, amekanusha madai kuwa alilieleza Bunge kuwa mkasa uliompata Kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari na Kamati ya kufuatilia haki zao, Dkt. Steven Ulimboka, kuwa alistahili, si ya kweli na KUOMBA RADHI madaktari nchini kwa jinsi alivyonukuliwa vibaya wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Bungeni tarehe 28 Juni 2012. Jana, Mbunge huyo alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa alisema, "kipigo alichopata Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dkt. Steven Ulimboka, kinastahili ili naye apate machungu wanayopata wagonjwa wengine mahospitalini."
Kauli hiyo ilisababisha tafrani kidogo bungeni, ambapo Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda alilazimika kuingilia kati kumzuia Ngonyani asiendelee kutoa kauli hiyo kwa vila suala la madaktari bado liko Mahakamani. | | |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇