Kutokana na kuendelea kwa mchakato wa uundwaji wa katiba mpya unaoendelea hapa nchini, taasisi mbalimbali, vyama vya siasa na mashirika, viongozi na hata makundi ya wasomi yamekuwa yakitoa mapendekezo ya uwepo wa vipengele mbalimbali vinavyoendana na mazingira ya sasa kiuchumi, kisiasa na utamaduni ili viwepo kwenye Katiba hiyo mpya.
Katika muendelezo huo, leo tarehe 13-06-2012 katika Ukumbi wa Eacronatal, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe, Maalim Seif Shariff Hamad ametoa hotuba katika Uzinduzi wa Kongamano la Muungano na Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.
Katika Hotuba yake hiyo, Mhe Makamu wa kwanza wa Rais alitoa shukrani zake za dhati kwa taasisi ya Ford Foundation yenye makao makuu yake New york nchini Marekani kwa kusaidia taasisi mbalimbali nchini Zanzibar tangu mwaka 1962 na pia kwa kufanikisha maandalizi ya kongamano hilo la kujadili katiba.
Aidha, Mhe. Makamu wa kwanza wa Rais,alieleza ukongwe wa mjadala wa Muungano ambao ulianza tuu baada ya muungano wenyewe, Lakini pia akapongeza juhudi za waasisi wa muungano na pia kusifu kuwa Muungano wetu unachukuliwa kuwa ni mfano kwa mataifa mengine hasa kwa kudumu kwake muda mrefu.
Pia, alibainisha kuwepo kwa manung'uniko mbalimbali katika muungano ambapo serikali imefanya juhudi za kuunda tume mbalimbali za kufuatilia juu ya manung'uniko hayo na kuyatafutia suluhisho lake.
".Alifafanua.
Mijadala hiyo inaendelea sehemu mbalimbali za Zanzibar na Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇