Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, kuongoza shughuli ya kuuaga mwili wa muasisi wa Chadema na Naibu Gavana wa benki kuu wa zamani, Bob Makani, leo. Wanaomkaribisha ni viongozi wa Chadema, Mwenyekiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk. Wilbrod Slaa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zitto Kabwe.
Rais Kikwete akiwa na viongozi wa Chadema, Mbowe, Dk. Slaa na Zitto Kabwe
Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba Mpya, Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba, na Waziri Mkuu mstaafu ambaye ni Mjumbe wa Tume hiyo, Dk. Salim Ahmed Salim, wakiwasili kwenye viwanja vya Karimjee.
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akimsalimia Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta
Mwenyekiti wa IPP, Reginard Mengi akisalimiana na Profesa Philemon Sarungi kwenye msiba huo
Dk. Slaa akimkaribisha Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye alipowasili kwenye msiba huo kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam
Kisha akamkumbatia
Rais Kikwete, Mbowe na Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal wakipokea mwili wa Bob ulipowasili Karimjee.
Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akitoa salama za CCM
Baadhi ya wanasheria wakiwa kwenye shughuli hiyo ya kuuaga mwili wa Bob Makani ambaye pia alikuwa mwanasheria wa siku nyingi; Picha zote na Bashir Nkoromo
Your Ad Spot
Jun 11, 2012
Home
Unlabelled
RAIS KIKWETE AONGOZA KUAGWA MWILI WA BOB MAKANI
RAIS KIKWETE AONGOZA KUAGWA MWILI WA BOB MAKANI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Undugu na utu wetu wetu hauwezi kutenganishwa na siasa..
ReplyDelete