LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 31, 2012

MDAU ANAOMBA MSAADA KWENYE TUTA KUHUSU VIONGOZI WA CHADEMA.

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe baada ya kushuka kwenye gari la bei mbaya
Mwananchi mwenzangu naomba msaada tutani!
Viongozi wa  CHADEMA waliwahi kutoa madai kwamba viongozi wa serikali iliyopo madarakani wanatumia magari ya bei mbaya sana, na ni gharama kubwa kuyahudumia, kwa maana ya vipuri, service na mafuta.
 Sasa swali ninalouliza ambalo naomba Watanzania wenzangu na wadau wengine popote duniani mnisaidie kupata jibu.Je.,mbona sasa na wao (Chadema) wanatumia magari kama hayo hayo wanayodai ni gharama kubwa???

Mnaweza kumjibu kwa kutoa Maoni kupitia ukurasa huu, au moja kwa moja kwenda kwake kwa mawasiliano haya hapa:-

PO BOX 33699,
HARBOUR VIEW TOWERS,
SAMORA AVENUE,
DAE ES SALAAM,
TANZANIA.
TEL + 255 22 2129550/1
FAX + 255 22 2129552
CELL + 255 784 721003
CELL + 255 752 721003

2 comments:

  1. kujidai kukataa magari ya bei ni janja tu ya aina ya siasa wanayoitumia (ujanjaujanja)"mapopulist" wanashadadia hoja nyepepesinyepesi ili mradi ziwapatie umaarufu. Sio ajabu hawa siku moja wakajadai IKULU wawe wanakula chukuchuku. WANAFIKI

    ReplyDelete
  2. Sikutegemea kusoma maoni ya namna hii kwenye blogu hii ya chama cha siasa! Nakiheshimu sana Chama cha mapinduzi, hivyo ningetegemea mtoa maoni (kukurukakara) aoneshe heshima ya CCM kwa kutotumia lugha yenye msamiati wa kejelei, kama vile "kujidai", "janja", "ujanjaujanja" na "chukuchuku". Chama kinachoongoza, kama "kukurukakara ni mwana-CCM au shabiki wa CCM, kiwafunde wanachama au mashabiki wake waoneshe adabu na staha kwa raia wenzao katika Jamhuri yetu hii sote!

    ReplyDelete

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages