Kumekuwepo matukio mbalimbali na kauli
ambazo kimsingi ni HATARISHI NA CHONGANISHI, mfululizo wa matendo na kauli hizi
umeshtua watanzania, wengi wakijiuliza ni nini hatma ya Taifa hili na mwenendo
wa kauli hizi za wapinzani. Kauli hizi ambazo wapinzani hasa viongozi
waandamizi na wadau wakuu wa CHADEMA wamekuwa wakizitoa kwenye hadhara
mbalimbali ambazo kwa upande mmoja unashutumu chama tawala kuhusika katika
mauaji ya viongozi wao.
Chadema wamekuja na mbinu mbaya na chafu za
propaganda za kukichafua chama cha Mapinduzi na hata kuwachafua viongozi wake
hadharani, na mbaya zaidi kutoa kauli zenye vitisho na zinazopanda mbegu ya
ubaguzi na uchonganishi baina ya watu wa Taifa hili kwa mlengwa wa dini zao na
kanda. Mara ya kwanza tulizisikia kauli kutoka kwa viongozi waandamizi wakisema
kuwa nchi hii haitatawalika, na watafanya kila watachoweza katika kulifanikisha
hilo, na mwingine muaasisi wa Chadema wakimshutumu Mwenyekiti baada ya kuunda
tume ya Katiba na sasa viongozi wengine wa chama hiki pinzani wananadi
hadharani kuwa wataigawa Tanzania na kujitangazia Uhuru kwa upande wa kaskazini
kwa mantiki kuwa huko ndiko lilipo chimbuko la Chadema na ndiko ambako chadema
inakujali na kujinasbisha nako.
Matukio ya vurugu ambazo zilitawala kila kona na hata mauaji ni matokeo
ya kauli hizi ambazo hazijawahi kukanushwa wala kusahihishwa kwa namna yeyote
ile kitu kinachopelekea tuamini kuwa dhamira hii ya viongozi hawa ni ya kweli-hawakukosea
kwa ulimi,ni dhamira endelevu.,na wanaifanyia kazi.,bila kujali madhara ya
kauli hiyo kwa jamii, ni wazi kuwa hii ni mikakati endelevu ya kuujumu nchi na
kufikia malengo yao haya ya kuhakikisha kuwa NCHI HII HAITAWALIKI., kama sivyo
kwanini haya hatukuyaona huko nyuma wakati vyama vingine vilipokuwa vyama vikuu
vya upinzani.,kwanini sura ya kitaifa imebadilika hivi sasa..,kama ccm ni ile
ile tangu kuanza kwa upinzani, sera zake, kanuni na hata katiba ni ile ile basi
ni wazi kuwa ni mabadiliko ndani ya upinzani ndio yamezalisha hali hii ya
kuchafua sura ya kitaifa hapa nchini kwa kauli na matendo.
Matendo na kauli za viongozi wa Chadema
zinanishawishi kuamini kuwa HAYA YANAYOENDELEA HIVI SASA NI MATOKEO YA MFUMO
MPYA NA MBAYA WA UPINZANI WA CHADEMA.,sisemi haya kwa kuwa mimi ni ccm hivyo
katika mlengwa wangu kisiasa ni kukipaka matope cdm bali nasema haya kwa
ushahidi wa kauli na wa matendo ya waaandamizi na watendaji ama viongozi wa
kitaifa wa chama cha chadema . Kauli hizi., hakika ni kauli mbaya sana kuwahi
kutolewa na kiongozi wa kisiasa na kitaifa tena ndani ya jukwaa mbele ya
halaiki ya watanzania.
Ukiwa Mtanzania mwenye uzalendo na utaifa juu ya nchi hii, laani kauli hii na mfano wa kauli hii ya Nassari. BOFYA HAPA
kiukweli kijana mwenzetu hajielewi.unajua mambo ya siasa yanahitaj kujipanga sasa viongozi waandamiz wa CHADEMA wanatumia vijana kama chambo katika kuupotosha umma wa vijana ambao wengi wao ni taifa la kesho,sasa hali hii ndio inayotokea kwa ndugu Nasari.Nikiwa kama kijana pia nachukua fursa hii kuwashauri vijana waache kupandikizwa mabaya na watu wachache wenye nia mbaya na taifa letu kwa maslahi yao na badala yake kuingia katika chama chenye misingi imara na maslah kwa wote....JIELEWE JOSHUA NA ACHA KUONGEA UJINGA KA UMMA
ReplyDeleteUmechemsha, watanzania sasa hawadanganyiki kwa misemo na kutunga story zisizo na mashiko, chadema hawawezi kuwabadilisha watanzania bali watanzania wamebadilika na dhahili wanahitaji mabadiliko yenye tija kwa nchi na si propaganda
ReplyDelete