Nimefuatilia kwa makini taarifa za magazetini leo na taarifa za mitandaoni juu ya Kauli ya Shibuda aliyoitoa Dodoma .
Ambapo alitoa kauli kuwa atawania nafasi yaUrais kwa tiketi ya Chadema mwaka 2015. Shibuda alisema hayo juzi mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kwenye semina iliyofanyika Dodoma katika ukumbi wa NEC ya CCM kuhusu utawala bora nchini iliyoandaliwa na taasisi inayotathmini utawala bora Afrika (APRM). Shibuda naye akiwa ni mjumbe wa Bodi ya Taasisi hiyo anayewakilisha vyama vya upinzani alikuwepo, akasema mbele ya Mweyekiti wa Semina hiyo Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
"Nakupa pole, kazi ya urais ni ngumu sana, bila shaka utakumbuka kuwa nami nilitaka kuwa mbadala wako, hata hivyo naamini utakuwa meneja wangu wa kampeni za urais mwaka 2015," alisema Shibuda. Rais Kikwete akamuuliza: " unataka urais kupitia chama gani?" Shibuda akajibu kwa kujiamini, "Kupitia Chadema, huku niliko sasa”.
Shibuda pia alizungumzia nafasi ya CCM katika siasa za Tanzania, na kukiri akisisitiza kuwa hivi sasa hakuna mbadala wa CCM katika kuongoza nchi akisisitiza kuwa CCM imejijenga kimfumo kuanzia ngazi ya juu mpaka kwenye mashina, jambo ambalo linarahisisha utoaji haki kuanzia chini mpaka juu.
Mbunge huyo, alisisitiza kuwa tatizo ndani ya CCM ni baadhi ya viongozi kuwa wabinafsi ambao aliwafananisha na kunguru wasiofugika, kwa kutofuata miiko na maadili ya chama na badala yake kuwa sehemu ya watu wanaoharibu chama hicho.
Baadaye, baraza la vijana la Chadema (BAVICHA) kupitia Mwenyekiti wake John Heche, walitoa tamko ambalo limeelezea hisia zao juu ya kauli hizo za Shibuda, kwa kueleza kushtushwa na mambo manne.
1. Eneo alipotoa kauli hiyo (NEC-CCM)
2. Meneja wa kampeni aliyemchagua (Rais Kikwete)
3. Kutokuwepo mbadala wa CCM katika uongozi wa Nchi
4. Kutoa kauli kwa niaba ya APRM.
Kisha wakaainisha mambo waliyodhani ni ya msingi katika kuikabili kauli hizo, kama ifuatavyo;
· Bavicha haitaruhusu Rai Kikwete kuwa meneja wa kampeni zao.
· Kamwe hairuhusu mgombea wake kutangaza nia kwenye vikao vya CCM.
· Chadema wamedai kudhalilishwa kwa kauli kuwa hakuna mbadala wa CCM kwa sasa,
· Shibuda anafanya nini Chadema ikiwa haendani na tamaduni zake???
· Wanawahakikishia vijana kuwa Chadema imejiandaa kuchukua nchi.
· Wanawandaa vijana kuwa tayari kumkabili “mtu” ambae ataonekana kuwa ni kikwazo kwa chama kuchukua dola 2015.
Mtazamo wangu:
Kwanza, Ni wazi kuwa hakuna namna kuwa wanachama wote wanaweza kuwa na mitazamo sawa na uwezo sawa wa kufikiri na kujenga hoja,lakini hii aina maana kuwa mwanachama mwenye mawazo tofauti na wengine kuwa mara zote amepotoka hasa ikiwa anazo hoja za msingi juu ya misimamo yake na mitazamo yake hiyo.
Kutokana na kauli hizi zilizotolewa na Chadema, kupitia midomo ya vijana wao ni wazi kuwa Tamko hili limetolewa kwa kukurupuka mno na bila kufanya tathmini ya kutosha na vilevile halikujali haki ya msingi ya Shibuda kama Mtanzania na mwanachama wa Chadema pia, kwa kuwa katika katiba ya nchi lakini pia katiba ya Chadema inaruhusu “mtu yeyote aliye mwanachama wa chama hiko anayo haki na fursa ya kuweza kuwa mgombea kupitia tiketi ya chama hiko” na katiba hiyo aianishi ni wapi sehemu pekee na rasmi ya kutoa kauli ya kutaka urais wa chama hiko labda bavicha wabainishe hili..,hivyo hakuna tatizo kwa mwanachama yeyote kutoa kauli kuwa atagombea urais sehemu ambayo anaona anaweza kuliongelea hilo, lakini kwa Chadema kufanya hivyo ni KOSA kwa “baadhi” ya wanachama wa Chadema ingawa katiba yao inaruhusu, siku za nyuma kidogo Mhe; Zitto Kabwe alijaribu na sokomoko lililomfika wote tunafahamu.
KWANINI IKO HIVI???
Hii ni kwa kuwa urais na uongozi wa juu wa Chama uko rasmi kwa watu Fulani tu, ni ajenda “iliyofungwa” ya watu ambao wamejipanga kuhakikisha kuwa milki ya Chama inabaki mikononi mwao milele na hivyo si sawa kwa mtu yeyote hata kutamani nafasi hiyo ya juu ya Chama.
Lakini hata mandhar ya kauli na kukuzwa kwake kunaashiria wazi kuwa kuna jambo liko nyuma ya Tamko hili kwani tamko la BAVICHA halikuzingatia pia, mandhar ya kauli hiyo ya SHIBUDA na maudhui yake halisi.
Lakini pia haiingii akilini kuwa mgombea wa kiti cha urais akapigiwa kampeni na mwenyekiti wa chama pinzani in real sense na Shibuda alilieleza hili kuwa ni utani na JK ni mtani wake, ingawa kwa vijana hawa walishikilia msimamo wao (weak stand + minor argument)
Pamoja na hayo, CDM wanajihisi kudhalilishwa na kauli ya shibuda juu ya kutokuwepo kwa mbadala wa CCM kwa sasa kwa namna ilivyojiimarisha katika mfumo wake ni ukweli usiopingika kuwa CCM iko kila kona ya Tanzania, kitongoji chochote, mtaa, kijiji, kata, tarafa na miji.
Kulingana na safu ya kiutawala na muundo wake unaoanzia Shina, CCM wanayo fursa ya kuwafikia wananchi wote wa ngazi za chini kabisa na hivyo kuweza kuwafikia watanzania wengi hasa wa vijijini, ambapo CDM wao wamejiimarisha zaidi maeneo ya majiji na kujipanga katika safu za mashambulizi dhidi ya CCM kupitia vyombo vya habari na kupitia kwenye mitandao, ambapo ni watanzania asilimia chache ambayo haizidi 10% wanapatikana huko. Na hili Shibuda ameliongea kutokana na ripoti hiyo ya APRM ambayo imefanya utafiti yakinifu katika hili (yeye akiwa miongoni mwa watafiti) bila shaka ameliongea hili kama mtafiti anayeelezea utafiti wake.
Tamko hili linaonyesha kukosa ukomavu wa kidemokrasia walionao watoaji wa tamko hili. Hivyo kudhihirisha kuwa bado wanahitaji muda katika kujifunza na kuielewa Demokrasia na siasa ya vyama vingi.
Hali ya Chadema katika maeneo ya kata, vitongoji na vijiji. Ofisi zimefungwa.
CDM hawajakomaa kisiasa. Isitoshe CDM haiwaheshimu Watanzania kwa sababu zifuatazo: Wakati wa kampeni za 2010, CDM, kwa uchu wao wa madaraka, walijaribu kuwadanganya wananchi kuwa eti wakitawala wao 1. Watatoa elimu bure kuanzia chekechea mpaka kidatu cha sita, 2. Tiba itakuwa bure kuanzia kumuona daktari, vipimo na dawa katika hospitali zote za serikali, na 3. Eti bei ya vifaa vitashuka bei kuliko hata gharama za uzalishaji wa vifaa hivyo huku kodi zote zikipunguzwa. Bahati nzuri Watanzania hawakukubali wala kuamini porojo hizo za Alnacha.
ReplyDeletekama si uchanga basi kuna kilichofichika kwani mara zote inaonekana kana kwamba wameamua kutumia siasa fulani zisizo za kiungwana Kujaza watu Kasumba, Chuki na Hasira.
ReplyDeleteNafikiri ndiyo mfumo wa SIASA za namna hiyo na kiukweli zina madhara makubwa kwani mtu kwa kawaida akiwa na hasira na chuki uwezo wa kufanya maamuzi sahihi hupungua.
Lakini kwa kuwa hasira za kupandikizwa si za kudumu, Baada ya mtu kutulia, kutafakari na kujihoji hugundua makosa hivyo kuacha kushabikia.
Maana yake WASIPOJIREKEBISHA siku zinakuja nazo si nyingi watapoteza kabisa UMAARUFU.
Waungwana hichi kinachotufanya kujenga hoja ili kufafanua juu uamuzi wa Shibuda ni nini? hivu kutokuelewa mazingira ya Shibuda kuzungumza kauli hiyo na hadi kufikia vijana wa Bavicha kulalamika ni kazi yetu kweli, hivi interesr yetu kwenye hili ni nini?
ReplyDeletenashauri mtandao wetu utumike kuweka vitu vyenye msingi na maslahi kwa chama chetu, hili sio miongoni mwao,kama vijana wa CDM wamekurupuka kumlaumu knogozi wao bila ya kumpa nafasi ya kujielelza na sisi tunaingia ili kujenga hoja kufafanua mazingira yalivyotokea Dodoma, huu ni udhaify wetu. Acheni DM waendele na tatioz lao la kupenda publicity ili waonekane kwamba na wao wapo. na sisi tusijiingize kucheza ngoma zao kwa ajili ya kuwafurahisha, hii tunaweza kuiona na saswa ama itampa unafuu Shibuda ila ukwlei ndio tunamjengea mazingira magumu zaidi kwa chama chake mana haingii akilini kwa mtu mzima aende kwenye cama cha wengine ili akaseme hoja yake, na kichaa yoyote anaelichukuwaa hili kwamba ndio hoja ya kumsulubu mwengine wka kisingizio chochote kile, huyo huwa tunamuita mwehu.
sasa acheni CDM iwehuke sisi tuendelee na kazi ya kujenga CCM na Nchi kwa ujumla wake.
kwetu sisi ni kuvua gwanda na kuvaa pamba ili tuzidi kupamba moto kwa maslahi ya watu wetu.