LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 14, 2022

MHARIRI MTENDAJI MSTAAFU WA UHURU/MZALENDO MZEE MUFUNGO AFARIKI DUNIA

 Na CCM Blog, Dar es Salaam

Mahariri Mtendaji mstaafu wa Magazeti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Uhuru na Mzalendo Mzee Josiah Mufungo, amefariki Dunia.


Taafa zimesema Mufungo amefariki usiku wa kuamkia leo na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Lugalo, Dar es Salaam.


Wakati akiwa Mhariri Mtendaji, magazeti ya Uhuru na Mzalendo yalikuwa yanachapishwa na Kampuni ya Uhuru Publications Limited, magazeti hayo sasa yanachapishwa na UMG ambayo inasimamia vyombo vya Habari vya CCM ikiwemo Uhuru fm.


Taarifa zaidi za msiba huu tutakuwa tunawahabarisha kupitia Blog hii ya Taifa ya CCM (CCM Blog).


Msimamizi Mkuu wa Blog hii kwa niamba ya timu nzima, anatoa pole za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo.

Mzee Josiah Mufungo enzi za Uhai wake.

1 comment:

  1. Dah Mungu amlaze pahali pema peponi amin. Ni mhariri wangu wa kwanza kuhariri habari zangu.

    ReplyDelete

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages