LATEST HEADLINES👉

Mar 29, 2020

NCHI 24 ZA AFRIKA ZAFUNGA MIPAKA KUZUIA KUENEA VIRUSI VYA COVID-19

Katika taarifa, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Afrika (Africa CDC), ambacho ni taasisi maalumu la Umoja wa Afrika, kimesisitiza kwamba nchi nyingine saba za Afrika zimeweka vizuizi vya kusafiri kutoka baadhi ya nchi. Aidha taarifa hiyo imeseba nyingine saba zimetoa maelekezo ya vizuizi vya kuingia nchini kwa wasafiri kutoka baadhi ya nchi.
Hali kadhalika  nyingi wanachama wa AU zimeweka karantini ya lazima kwa wasafiri wote au wasafiri wanaofika kutoka maeneo yenye hatari kubwa zaidi. Hata hivyo taarifa hiyo imesisitiza kuwa nchi za Afrika zinaruhusu mizigo, shehena na usafiri wa dharura kuingia ndani na kutoka nje ya nchi.Wakati huohuo Africa CDC pia imebainisha kwamba idadi ya vifo vinavyotokana na COVID-19 katika bara la Afrika imefikia watu 83 na wagonjwa waliothibitishwa wamezidi 3,243 kufikia siku ya Ijumaa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages