LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 12, 2019

MRTIN FAYULU AWASILISH KESI YA KUPIGA USHINDI WA FELIX TSEKEDI

Martin Fayulu, mgombea urais kupitia muungano wa upinzani wa Lamuka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amewasilisha kesi katika Mahakama ya Katiba kupinga, ushindi wa Felix Tshisekedi, aliyetangazwa wiki hii na Tume ya Uchaguzi kuwa alishinda uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 30 mwezi Desemba mwaka jana.
Wakili wa Fayulu, Feli Ekombe amewaambia wanahabari jijini Kinshasa kuwa, mgombea huyo anataka matokeo yaliyompa ushindi Tshisekedi, yafutwe.
Tume ya Uchaguzi ilimtangaza Tshisekedi mshindi, kwa kupata asilimia 38.57 ya kura zote zilizopigwa huku Fayulu akiwa wa pili kwa asilimia 34.8.
Mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shadary, aliambulia asilimia 23.8.
Hata hivyo, Fayulu tayari amesema alishinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 61 ya kura zote.
Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, waliokuwa na waangalizi zaidi ya 40,000 kote nchini humo, limesema matokeo yaliyotangazwa hayakuwa sahihi.
Felix Tshisekedi, aliyetangazwa mshindi wa kiti cha urais
Kauli hii ya Kanisa Katoliki, imeungwa mkono na mataifa ya magharibi kama Ufaransa, Uingereza, Ubelgiji huku Marekani ikisema inataka ukweli kufahamika. 
Wakati uo huo, vyama vya siasa vinavyomuunga mkono rais anayeondoka madarakani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila vimenyakua viti vingi katika uchaguzi wa Bunge.
Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (CENI), vyama hivyo vimenyakua jumla ya viti 288 kati ya 429 Bungeni, huku vyama vya upinzani vikiambulia viti 141 tu.
Kwa mujibu wa sheria, chama au muungano wa vyama unaopata zaidi ya viti 250 ndio wenye sauti na ambao utakuwa na ushawishi wa kulidhibiti Bunge hilo la DRC kwa miaka mitano ijayo

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages