LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 30, 2018

WAPINZANI MADAGASCAR WATAKA KURA ZA UCHAGUZI WA URAIS ZIHESABIWE TENA

Wafuasi wa kambi ya upinzani nchini Madagascar wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo, Antananarivo wakitaka kuhesabiwa tena kura za uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni nchini humo.
Maandamano hayo yamefanyika siku mbili baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Madagascar kumtangaza Andry Rajoelina kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi wa rais. Waandamanaji hao wamesema kura za uchaguzi wa rais zinapaswa kuhesabiwa tena na kubaini nani mshindi halisi wa uchaguzi huo. 
Maelfu ya wafuasi wa Marc Ravalomanana aliyewahi kuwa rais wa Madagascar wametoa wito wa kufutwa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuwatuhumu wajumbe wa tume hiyo kuwa wamefanya udanganyifu. 
Matokeo yaliyotangazwa na tume hiyo yameonesha kuwa, Meya wa zamani wa Antananarivo  Andry Rajoelina ndiye aliyepata kura nyingi zaidi katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais iliyofanyika mwezi huu wa Disemba 19. 
Marc Ravalomanana amepinga matokeo ya uchaguzi wa rais Madagascar.
Kwa mujibu wa tume hiyo, Andry Rajoelina, ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 55.66 ya kura, huku Marc Ravalomanana akipata asilimia 44.34 ya kura.
Kabla ya kutangazwa matokeo hayo ya muda, marais hao wa zamani wa Madagascar kila mmoja alijitangaza mshindi wa uchaguzi huo, siku moja baada ya zoezi hilo la Disemba 19. 
Mahakama Kuu ya Katiba ya madagascar ina siku tisa kuanzia Alkhamisi iliyopita kuthibitisha matokeo hayo ya muda yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya kisiwa hicho cha kusini mashariki mwa bara Afrika. 

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages