LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 5, 2018

WATU 33 WAFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA EBOLA MASHARIKI MWA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO

Watu wasiopungua 33 wanaripotiwa kufariki dunia kwa ugonjwa wa Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, siku chache baada ya maambukizi ya ugonjwa huo hatari kuripotiwa tena nchini humo.
Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema katika taarifa yake rasmi kwamba, maambukizi mapya ya ugonjwa hatari wa Ebola yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 33, mashariki mwa nchi hiyo.
Mbali na vifo hivyo, Wizara ya Afya ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa, kuanzia tarehe Mosi ya mwezi huu wa Agosti, maambukizi mapya  13 yameripotiwa katika jimbo la Kivu Kaskazini.
Hata hivyo, serikali ya DRC inasema kuwa, inashirikina na maafisa wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kutoa elimu kwa wakazi wa mashariki mwa nchi hiyo ili kuepusha maambukizi mapya.
Maambukizi mapya ya Ebola yaliripotiwa katika wilaya ya Mangina, yapata kilomita 30 kutoka mjini Beni, wiki moja baada ya serikali ya Kinshasa kutangaza kuwa hakukuwa na maambukizi mapya kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.
Mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola uliripotiwa tarehe 8 Mei mwaka huu katika mji wa Bikoro mkoani Ă‰quateur kaskazini magharibi mwa DRC na baadaye ukaenea kwenye mji wa Mbandaka katikati mwa mkoa huo.
Watu zaidi ya 11,300 walifariki dunia katika nchi kadhaa za magharibi mwa Afrika kuanzia mwaka 2013 hadi 2016 kutokana na kuugua ugonjwa huo. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Liberia, Guinea na Sierra Leone zimeathirika sana kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages