LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 28, 2018

17 WAUAWA KATIKA MAPIGANO YA KIKABILA NCHINI MALI

Watu wasiopungua 17 wameuawa katika mapigano ya kikabila katikati mwa Mali huku uchaguzi wa rais ukikaribia katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.
Taarifa zinasema mapigano hayo yalitokea Ijumaa usiku katika kijiji cha  Somena karibu na mji wa Djenne katika mkoa wa Mopti kati mwa mali. Taarifa zinasema mapigano hayo yamejiri kati ya makabila ya Dozo na Fulani.
Mapigano hayo yamejiri wakati uchaguzi wa rais unatazamiwa kufanyika kesho Jumapili ambapo wapiga kura watachagua baina ya wagombea 24 akiwemo Rais wa sasa Ibrahim Boubacar Keita ambaye aliingia madarakani mwaka 2013 huku mgombea mkuu wa upinzani akiwa ni Soumaila Cisse.
SoumaĂŻla Cisse mgombea urais Mali
Nchi ya Mali ilikumbwa na ghasia na ukosefu wa amani baada ya mapinduzi yaliyotokea nchini humo mwaka 2012. 
Askari wa Umoja wa Mataifa maarufu kama MINUSMA walitumwa nchini Mali mwaka 2013 lakini wameshindwa kurejesha amani na utulivu katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages