LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 19, 2017

UTENGANISHAJI WA UPEPELEZI NA UENDESHAJI KESI UMEKUWA NA TIJA

Na Mwandishi Maalum,
Mkurugenzi wa Mashtaka  Bw. Biswalo Magaga, (DPP) amesema , utekelezaji wa mpango wa Serikali wa kutengenisha  jukumu la  upepelezi na  upelelezi   mashataka umekuwa wa mafanikio makubwa yakiwamo yakupunguza mlundikano wa  mahabusu.

Mkurugenzi wa Mashtaka ameyasema hayo wakati alipokuwa akielezea utekelezaji wa mpango huo  tangu ulipoanzishwa  kwa  sheria ya   mfumo wa mashtaka 2007,mbele ya  wajumbe wa Baraza la  Wafanyakazi wa Ofisi ya  Mwanasheria  Mkuu wa  Serikali linalokutana kwa siku mbili mkoani Dodoma.

“ Tangu kuanza kwa mpango huu  tumepata mafanikio makubwa, kwani  kwa sasa kumekuwa na wafungwa wengi kuliko mahabusu  kwa maana kwamba idadi ya mahabusu imezidi kwa 2000  kama ilivyo kuwa huko nyuma ”. Akabainisha  Mkurugenzi wa Mashtaka.

Mpango wa serikali wa kutenganisha  shughuli  za upelelezi na  mashtaka  ulilenga  kuondoa tatizo la haki kuchelewa kutendekea na kesi kuchukua muda mrefu mahakamani kwa sababu ya muda mrefu unaotumika katika upelelezi.

Mafanikio mengine kwa mujibu wa  Mkurugenzi wa Mashtaka  ni jamii kurejesha imani kwa vyombo vya sheria  kutokana na haki kutendeka  na kwa wakati na hivyo kupunguza  vitendo vya wananchi kujichukulia hatua mkononi.

Mafanikio mengine   kesi zinazoendeshwa  na  Mawakili wa Serikali  zimekuwa na mafanikio makubwa ikilinganishwa na zile ambazo  zinasimamiwa na  mawakili wakujitegemea. Kiasi cha kusababisha kupunfua kwa  ukataji wa rufaa na mashauri ya jinani  kupugua  kutokana na jamii kutambua uhalifu haulipi.

“ Kutokana na utekelezaji wa mpango huu,  siyo tu kumepunguza  rufani zinazopelekwa  Mahakama ya  Rufaa kwa wakata  rufaa kupungua  kutokana na weledi wa mawakili na kazi kubwa na nzuri wanayoifanya ya kuiwakilisha serikali Mahakamani”.Amebainisha  Mkurugenzi wa Mashtaka.

Akaongeza pia kwamba  hata  barua za malalamiko kutoka kwa wananchi zimepungua  kiasi kwamba mafaili hayajai  tena barua za malalamikio kama ilivyokuwa huko nyuma na hiki ni   nikielelezo kikubwa kwamba wananchi wanapata huduma za kisheria  kwa ufanisi  mkubwa” akasisitiza Mkurugenzi wa Mashtaka. 

Pamoja na mafanikio hayo, Mkurugenzi wa Mashtaka ameelezea baadhi ya  changamoto  ni kutokuwapo kwa  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika    baadhi ya  Wilaya  hususani katika  baadhi  ya Wilaya ambazo zinamtukio mengi ya jinai.

Amesema ufinyu wa bajeti na upungufu wa raslimali watu  ndiyo unaochangia au kurudisha nyuma kasi ya  ufunguzi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kila wilaya ili kuwafikishia huduma kwa karibu wananchi.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Mashtaka  ametoa rai kwa  Mawakili  Wafawidhi   pamoja na  Mawakili wote kutekeleza  majukumu yao ya kuisimamia  Serikali bila woga na kwa kuzingatia maadili na weledi na wasikubali kuyumbishwa.


“Tekelezeni majukumu yenu kwa mujibu wa taaluma yenu, msiogope kusimamia ukweli na kile mnachokiamini katika utekelezaji wa majukumu yenu”. Akasisitiza  Mkurugenzi wa Mashtaka.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages