Friday, October 6, 2017

MKUTANO MKUU WA CCM WILAYA YA KINONDONI, LEO, MCHUANO MKALI WA WAGOMBEA WATIKISA UKUMBI

 Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni Hanaf Msabaha akifungua Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, uliofanyika leo Kinondini Vijana Social Hall. Mkutano huo umefanyika kwa ajili ya kutoa fursa kwa wajumbe wa mkutano huo kupiga kura kuwachagua viongozi wapya wa Chama akiwemo Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya na pia Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.
 Msimamizi wa Uchaguzi huo Ramadhani Shabani akizungumza kabla ya uchaguzi kuanza
 Wajumbe wakinyoosha mikono kuunga mkono moja ya maamuzi wakati wa mkutano huo wa uchaguzi
 Wajumbe wakifuatilia hatua kwa hatua maamuzi wakati wa mkutano huo wa uchaguzi
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Tungaraza akizungumza baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Uchaguzi kwenye Mkutano huo
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akisalimiana  na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Salum Hapi baada ya kuwasili kwenye mkutano huo
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Alhaj Abdallah Bulembo akizungumza baada ya kupewa nafasi kwenye mkutano huo
 Wagombea wa nafasi ya mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ki8nondoni wakiwa tayari kuomba kura. Wagombea hao kutoka kushoto  ni John Mome Morro, Harold John Maruma, Khalid Huma Sindano, na  Emmanuel Josph Mbasha.

 Wagombea wa nafasi ya Mkutano Mkuu wa CCM wakiwa tayari kuomba kura 
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

CCM Blog. Powered by Blogger.