LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 1, 2017

RAIS DK. MAGUFULI AMUAGA WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA ALIYEKUWA HAPA NCHINI TANGU JANA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza  mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn kwenda kuangalia vikundi vya ngoma za asili kabla ya kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kurejea nchini kwake mara bada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn wakati wa nyimbo za mataifa mawili ya Tanzania na Ethiopia zikipigwa uwanjani hapo kabla ya mgeni huyo kuondoka jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn kabla ya kupanda ndege na kuondoka jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakijadiliana jambo mara baada ya Rais Dkt. Magufuli kuchangia vikundi mbalimbali vilivyotumbuiza uwanjani wapo wakati wageni mbalimbali wanapowasili kiasi cha Tsh. Milioni 15 kama kuthamini mchango wao wanaoutoa. Pia Waziri Mkuu Majaliwa aliwachangia kiasi cha Tsh. Milioni 5. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

 Vikundi mabalimbali vya ngoma pamoja na ushereheshaji vikishangilia wakati Rais Dkt. John Magufuli pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa walipokuwa wakizungumza kuhusu Serikali kuthamini mchango wa vikundi hivyo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakitoka kumsindikiza Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn ambaye ameondoka mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wakizungumza na washereheshaji pamoja na vikundi mbalimbali vya ngoma  uwanjani hapo (JNIA). Wakwaza kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages