GEREZA KUU NCHINI RWANDA LATEKETEA KWA MOTONO MJINI KIGALI

Gereza kuu la Kigali maarufu 1930
Gereza kuu la Kigali maarufu 1930
Gereza kuu la Kigali maarufu 1930 lateketea kwa moto. kufikia jana jioni moshi ulikuwa bado unaendelea kutanda huku kilichosababisha moto huo kikiwa bdo hakikajulikana.

Shughuli za kuzima moto zilikuwa  bado zinaendelea huku vikosi vya Askari Jeshi na polisi vikionekana hapa na pale kando kando mwa jengo la gereza hilo.

Hilo ni gereza linalohifadhi wafungwa mchanganyiko wakiwemo wale wa kisiasa na wengine wa mauaji ya kimbari.

Miongoni mwa wafungwa wa kisiasa ni Victoire Ingabire aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela miaka minne iliyopita kwa hatia ya kuchochea utengano wa kikabila na kuhatarisha usalama wa raia.

Viongozi kadhaa serikalini wakiwemo mawaziri na wakuu wa majeshi na ulinzi na polisi wamefika kwenye eneo la tukio

Bado ni mapema kujua athari zilizotokana na tukio hilo kwani waandishi wa habari hawajaruhusiwa kuingia katika jengo la gereza hilo kuu ya Kigali.

Magari ya zima moto bado yanapishana na magari ya kubeba majeruhi huku wafungwa wakionekana nje ya gereza na ulinzi ukiwa umeimarishwa. BBC

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.