Sunday, October 9, 2016

RAIS DK MAGUFULI AMTEUA MHANDISI KILABA KUWA MKURUGENZI MKUU MPYA TCRA

Mhandishi James Mtayakingi Kilaba
DAR ES SALAAM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli, amemteua Mhandisi James Mitayakingi Kilaba kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na kusambazwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Dar es Salaam, imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi James Mitayakingi Kilaba umeanza jana, Jumamosi, Oktoba 8, 2016.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi James Mitayakingi Kilaba alikuwa akikaimu nafasi hiyo, baada ya uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dk. Ally Yahaya Simba kutenguliwa.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.