Thursday, September 15, 2016

ZENDA: MBOWE, MBATIA MSITAFUTE UMAARUFU KUPITIA JANGA LA TETEMEKO LA ARDHI, AIPONGEZA SERIKALI KWA HATUA ZA HARAKA

Daniel Zenda
Na Mwandishi Wetu
Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, limetoa pole kwa wale wote waliokumbwa na kuathirika na maafa ya janga la tetemeko la ardhi yaliyotokea katika mkoa wa Kagera, na baadhi ya sehemu za mikoa ya mwanza na Shinyanga.

Pamoja na pole hizo, Shirikisho hilo, limempongeza Rais John Magufuli na Serikali yake kwa jumla, kwa kuchukua hatua za haraka kwa kuonyesha utayari na uharaka katika kuwasaidia walioathirika na janga hilo.

"Tungependa kumpongeza kipekee, Mheshimiwa Rais kwa kuguswa na jambo hil, kiasi cha kuamua kuahirisha ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchi Zambia, ikiwemo kuhudhuria kuapishwa kwa Rais mpya wa Nchi hiyo", . 

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam, na Mkuu wa Idara ya Mambo ya Nje na Mahusiano ya Kitaifa na Kimataifa wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, Katibu Msaidizi wa CCM,  Daniel Zenda.

Amesema, pia Shirkisho linawapongeza wadau na watanzania wote kwa jumla waliojitokeza kwa haraka na wanaoendelea kujitokea hadi sasa kusaidia kwa namna mbalimbali wanachi walioathiriwa na janga hilo la tetemeko la ardhi, lililotokea Septemba 10, mwaka huu. 

Zenda amesema Shirikisho pia linatoa rai kwa wanasiasa kuacha kulitumia janga hilo  la tetemeko la ardhi kama fursa ya kujijenga na kutafuta umaarufu wa kisiasa.

"Shirikisho linawataka wanasiasa wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia kuacha kutumia janga hilo kuchonganisha wananchi na serkali yao ambayo imeshaanza kuchukua hatua za muda mfupi na mrefu ikiwemo kuhakikisha waathirika wanapata makazi, chakula na mali walizopoteza kutokana na janga hilo", alisema Zenda.

Zenda ametoa mwito kwa walioathirika kuendelea kuwa na shubira kwa kuwa serikali imeshaanza na inaendelea kuwa karibu nao katika kuhakikisha hali yao inarejea katika mazingira bora kufuatia janga hilo ambalo  lilikuwa la dharura.

Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.