Thursday, September 15, 2016

MSEMAJI WA CCM NDG OLE SENDEKA ASHIRIKI MAZISHI YA MWANASIASA MKONGWE WA KENYA MAREHEMU WILLIAM OLE NTIMAMA

Msemaji wa CCM Mhe Christopher Ole Sendeka (kulia) akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe Uhuru Kenyatta walipokutana katika mazishi ya Mwanasiasa Mkongwe marehemu William Ole Ntimama yaliyofanyika Narok nchini Kenya, jana.

Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Christopher Ole Sendeka ameshiriki mazishi ya mwanasiasa mkongwe nchini Kenya marehemu William Ronkurua Ole Ntimama yaliyofanyika jana nchini Kenya.

Marehemu Ole Ntimama ni mwanasiasa aliyetumikia kwa muda mrefu ambaye ametumikia Kenya akiwa kama Mbunge kwa miaka 25 akiwakilisha jimbo la Narok na katika miaka yake hiyo amekuwa Waziri katika Serikali ya Mzee Daniel Arap Moi na Mzee Mwai Kibaki.

Katika wasifu wake marehemu anatajwa kuwa ni mwanaharakati na mpambanaji wa haki za wafugaji wa kabila la Maasai tangu katika kipindi cha awamu ya kwanza ya Hayati Mzee Jomo Kenyatta. Alianza kushiriki siasa kwa kugombea na kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Jimbo la Narok mwaka 1974.

Baada ya Kenya kujiunga na mfumo wa siasa ya Vyama vingi miaka ya 1990, Mhe Ntimama alikuwa kinara na msemaji wa chama cha KANU katika mapambano ya vyama vingi ingawa alijiunga na chama cha Democratic Party - DP chini ya Kibaki na baadae kujiunga na Orange Democratic Party - ODM na kushiriki uchaguzi wa mwaka 2007 ambapo alichaguliwa kuwa Mbunge wa Narok kwa mara nyingine mpaka mwaka 2013.

Alitangaza kustaafu siasa rasmi tarehe 14 Septemba 2014 lakini mpaka umauti unamfika nyumbani kwake Narok Marehemu Ole Ntimama alikuwa ni mfuasi na mwanasiasa mkongwe mwenye ushawishi ambaye anamuunga mkono kwa kiasi kikubwa Rais wa Kenya Mhe Uhuru Kenyatta.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.