ALIYEKUWA MKURUGENZI WA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA, ATINGA KIZIMBANI LEO, JIJINI DAR ES SALAAM

 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu (Pichani), leo amefikishwa katika Mahakama ya hakim Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, akiwa na wafanyazi wengine wa Mamlaka hiyo.

January 2016, Rais Dk. Magufuli Magufuli alitengua uteuzi wa Mkurugenzi huyo na kumsimamisha kazi yeye na wafanyakazi wengine kadhaa kupisha uchunguzi wa namna NIDA ilivyotumia kiasi cha sh. bilioni 179.6, katika kazi ya upatikanaji wa vitambulisho vya taifa wakati huku kukiwa bado kuna malalamiko kwamba watu wengi walikuwa hawajapata vitambulisho hivyo.
Maimu  (watatu kushoto) akiwa na wenzake katika Mahakama hiyo, baada ya kufikishwa leo

0 comments:

Post a Comment

Mdau, Uwanja huu ni wako, Toa maoni yako yasaidie kujua wewe unafikiri nini kifanyike kuboresha zaidi maisha ya Watanzania. Maoni yako yasilenge kuchochea mtafaruku katika jamii, kisiasa, kidini, kikabila au kijinsia. Mawasiliano yetu:- simu +255 (0) 712 498008, Email: nkoromo@gmail.com.
Bashir Nkoromo
Msimamizi Mkuu, Blog ya Taifa ya CCM.