LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 25, 2016

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA KAMISHNA MKUU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA MTENDAJI MKUU WA HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye kuwa Kamishna Mkuu wa Jeshi la Zimamoto nchini.
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Aprili, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Kamishna Andengenye umeanzia leo tarehe 25 Aprili, 2016.
Kamishna wa Polisi Andengenye anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Pius Makuru Nyambacha ambaye amestaafu.
Kabla ya uteuzi huo Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye alikuwa Kamishna wa Utawala na Utumishi, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Donan Mmbando kuwa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages