Saturday, July 18, 2015

RAIS WA ZANZIBAR, ALHAJI DK. SHEIN AONGOZA WAISAM KATIKA SWALA YA EID ELHAJ NA BARAZA LA EID LEO MJINI ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma ya gwaride maalum la kikosi cha Polisi FFU leo wakati wa Baraza la Idd katika Kusherehekea Sikukuu ya Idd el Fitri, Sherehe za Baraza Idd lilifanyika ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein(wa pili kulia) akijumuika na Viongozi na waislamu mbali mbali katika swala ya Suna ya Idd el Fitri iliyoswaliwa kitaifa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein(wa pili kulia) akijumuika na Viongozi na waislamu mbali mbali katika swala ya Suna ya Idd el Fitri iliyoswaliwa kitaifa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja
 Waislamu wa mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja wakimsikiliza Sheikh Soraga(hayupo pichani) alipotoa hutba ya swala ya Idd el Fitri leo  iliyoswaliwa kitaifa   katika viwanja vya Maisara Suleiman,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi na wananchi wakiitikia Dua iliyoombwa na Kadhi Mkuu wa zanzibar Sheikh Khamis Haji baada ya kumalizika kwa Swala na Hutba katika viwanja vya Maisara Suleiman leo,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Viongozi na Mashekhe waliofika Ikulu Mjini Unguja leo kwa madhumuni ya kupokea mkono wa Idd na kusoma Dua katika Sikukuu ya Idd el Fitri inayoadhimishwa Duniani kote. Kulia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akitoa Mkono wa Iddi kwa wananchi mbali mbali waliofika  viwanja vya Ikulu mjini Unguja leo katika kusherehekea Sikukuu ya Idd el Fitri
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein akitoa hutuba yake wakati wa sherehe za Baraza la Iddi el Fitri zilizofanyika leo katika ukumbi wa Salama bwawani Hotel Mjini Unguja,
Baadhi ya Wake wa Viongozi na wananchi mbali mbali wakisikiliza hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein aliyoitoa leo katika kusherehekea Sikukuu ya Idd elFitri katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.