LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 16, 2015

KAMATI KUU YA CCM KUKUTANA TAREHE 22 MEI


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habar katika ofisi za CCM makao  makuu jijini Dar es salaam wakati akizungumzia kusogezwa mbele kwa vikoa vya Halmashauri Kuu na Kamati Kuu.(PICHA NA KIKOSIKZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM) 2 
Nape Nnauye akisisitiza jambo katika mkutano huo wakati wa mkutano huo. 3 
Baadhi ya wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
…………………………………………………………………………….
Chama cha Mapinduzi kinatarajia kufanya vikao vyake mjini Dodoma ambapo tarehe 22 Mei kitafanyika kikao cha Kamati Kuu ya CCM ambapo tarehe 23 na 24 kutakuwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Katibu wa Nec,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye,amesema sababu ya kuahirisha vikao hivyo ni kupisha ratiba ya vikao vya baraza la wawakilishi vitakavyoanza Mei 18 mwaka huu. ”Vikao vya baraza la wawakilishi vitaanza Mei 18 hadi 21,vikao hivi ambavyo vitafanyika mfululizo vitatoa ratiba ya wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais wa Zanzibar,Wabunge na Baraza la Uwakilishi,”amesema Nape Nape alisema ratiba hiyo itawezesha wagombea kujitangaza na kuchukua fomu kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages