Monday, January 12, 2015

MBUNGE WA MCHINGA AWAPONGEZA WANANCHI WA KIJIJI CHA KILANGALA B KWA KUICHAGUA CCMKatibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akitoa salaam za pongezi kwa wananchi wa kijiji cha Kilangala B kata ya Kilangala  kwa kuipa ushindi CCM kwenye uchaguzi serikaliza mitaa uliofanyika desemba 2014, Katika mkutano huo Nape aliwaeleza wananchi hao CCM ndio chama pekee kinachotoa majibu kwa matatizo ya wananchi.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Mwenyekiti  aliyeshinda uchaguzi Hamid Rashid Namtonda akitoa salaam za kushukuru wakazi wa kijiji cha Kilangala B kata ya Kilangala jimbo la Mchinga.
 Mwenyekiti wa kijiji cha Kilangala B akiwashukuru wananchi wake kwa kumchagua kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ,vijiji na vitongoji uliofanyika desemba 2014.
 Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mheshimiwa Said Mtanda akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Kilangala B wakati wa kumtano wa kuwashukuru na kuwapongeza wananchi wa kijiji hicho kuichagua CCM, mkutano huu ulifanyika tarehe 11 Januari 2015.
 Wananchi wakisikiliza salaam za shukrani kutoka kwa Viongozi wao.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.