Tuesday, January 13, 2015

KAMATI KUU YAKUTANA ZANZIBAR


 Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kwenye Afisi Kuu ya CCM Zanzibar tayari kwa kikao cha  Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete   akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai leo alipofika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja  akihudhuria Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa(katikati) Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana .
 
 Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana katika viwanja vya Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo walipohudhuria katika Kikao cha kawaida cha siku moja cha Kamati Kuu ya CCM Taifa.


 Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Mjumbe wa Sekretarieti ya Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Haji Mkema mara alipowasili Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo alipohudhuria katika Kikao cha kawaida cha siku moja cha Kamati Kuu ya CCM Taifa (wa pili kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana (kushoto).
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akisalimiana na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Mjumbe wa Kamti Kuu ya CCM Taifa Dk.Mohammed Gharib Bilali wakati alipowasili Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja leo katika Kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.


Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.