Sunday, November 16, 2014

UKAWA WAHAMIA CCM IRINGA

Mbunge  wa  jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa kulia akipokea kadi ya Chadema  kutoka kwa mmoja kati ya  viongozi wa Chadema   kata ya Lyamgungwe  aliyehamia CCM
Mbunge Mgimwa  akikagua miradi ya maendeleo  jimboni kwake
Wananchi  wa Lyamgungwe  wakiwa  wameongozana na mbunge wake  kwenda kutembelea  miradi ya maendeleo
Kada  wa Chadema  kulia akipongezwa na mbunge Mgimwa baada ya  kujiunga na CCM
Mbunge Mgimwa akizungumza na  wananchi  wake baada ya  kupokea  wana chama wa Chadema

Na MatukiodaimaBlog
VIONGOZI  watatu  wa vyama  vinavyounda katiba ya  wananchi (UKAWA) kata ya Lyamgungwe  jimbo la kalenga  wamempongeza mbunge wa  jimbo la hilo Godfrey Mgimwa   kwa  kutekeleza ahadi  mbali mbali  zilizoachwa na marehemu mbunge aliyepita Dr  Wiliam Mgimwa kwa  muda mfupi na kuwa katika  kuonyesha  umoja  wao wameamua  kuunganisha  nguvu zao  kwa  mbunge huyo kwa kuhama Chadema na  kujiunga na CCM.

Akizungumza  kwa niaba ya  wanachama  wenzao zaidi ya 20 ambao  walikuwa nyuma  yao kabla ya   kujiengua  Chadema na  kujinga na CCM   walisema kuwa  sababu ya  kujiunga na upinzani  ilitokana na makundi  ndani ya CCM na upendeleo wa uteuzi wa wagombea  mbali mbali pamoja na wabunge  waliotangulia  kuonyesha kutumia ubunge kulea  familia  zao badala ya kuleta maendeleo  katika jimbo  hilo jambo ambalo mbunge Mgimwa amekuwa wa  tofauti  na  wabunge wengine kwa kuonyesha  kuwajali  zaidi  wapiga kura  wake .

Bw Mapinduzi Kalolo  ambae  alikuwa ni    viongozi  wenzake  wengine  waliorudi CCM ni  pamoja na katibu kata ,mwenyekiti na wajumbe na  kuwa  kujiunga kwao  Chadema  ni baada ya mambo  ndani ya CCM kutokwenda  vizuri  ila kwa  sasa  mbunge  wao  ameendelea  kuwaunganisha   wananchi  wote  bila  kujali itikadi zao  za  vyama .

Pia alisema  walipotoka CCM kwenda  Chadema  walikuwa  wameahidiwa mambo  mengi na viongozi wa Chadema jimbo  hilo la Kalenga  ila baada  ya  kujiunga utekelezaji wa ahadi  walizotoa  ikiwemo ya  kufungua ofisi  ilionekana na ngumu na kuwa  chama  hicho hata  kuwajali kilishindwa na  hivyo kuishia  kuonekana si chochote katika kata  hiyo  zaidi ya  kutumika kama karai na Chadema.

"Kujiunga na  Chadema  kweli  tulikuwa  tumepotea  ila  kwa  sasa  tumeona  ni vema  kurudi  kwa  baba na mama  CCM baaba  ya maisha ya  kuishi kama mwana mpotevu  kutushinda ...... hivyo tunakuhakikishia  mheshimiwa  mbunge Mgimwa  wewe  ndio  umetushawishi  kuhama  Chadema na kujiunga na CCM kutokana na kuonyesha mfano katika kutekeleza ahadi  zao kwa  wananchi .....kalenga hatujapata  kuwa na mbunge ambae  amefanya mambo makubwa kama wewe  ndani ya  miezi minne ...haya  uliyofanya  wewe  wabunge wengine  walikuwa  wakishindwa  kuyafanya kwa  kipindi  cha miaka 5  ya  ubunge "

Hata    hivyo  Kalolo  alisema  kuwa  ni matumaini makubwa  kwao  kuwa  kazi iliyofanywa na mbunge Mgimwa kwa  kipindi  kifupi  cha miezi  minne  ama  cha mwaka  mmoja wa utawala  wake ni imani  tosha kwao kwa  kuendelea  kumchagua  zaidi kwa  miaka mingine 10  mbele  ili  kuliwezesha  jimbo  hilo  kuwa la mfano zaidi.

HIvyo alikitaka   CCM kuacha tabia ya  viongozi  wake wa  wilaya  kuwaruhusu  baadhi ya  wana CCM kuzunguka  kuwavuruga wapiga  kura  kwa  kubeza jitihada  zinazofanywa na mbunge  Mgimwa na kuwa kufanya  hivyo ni  kukaribisha upinzani katika   jimbo  hilo.

Kalolo  alisema  iwapo  viongozi wa CCM ngazi ya  wilaya na mkoa  watashikamana na mbunge  Mgimwa upo  uwezekano  wa upinzani kufutwa kabisa katika jimbo  hilo ambalo halijapata  kuwa na historia ya  kuongozwa na upinzani .


kwa  upande  wake  aliyekuwa  mwenyekiti  wa  jimbo  la  kalenga kupitia  Chadema  Dr  Salum Kalolo  alisema  kuwa  kuondoka kwa   viongozi hao  Chadema na  kujiunga  na CCM kutokana na utendaji wa  mbunge  huyo Mgimwa hawajakosea kwani kwa  mtazamo  wake  kazi inayofanywa na mbunge  huyo jimboni inapaswa  kuungwa mkono na  kila mwananchi bila kujali itikadi ya chama chake.

" Wengi  walijua kuwa  kutokana na ujana  wake  mambo ya maendeleo  yasingeweza  kusonga mbele  ila mimi  si CCM mimi ni Chadema kutoka  sakafu ya  moyo  wangu  ninampongeza munge Mgimwa  amekuwa mbunge wa  mfano katika  kutuletea maendeleo Kalenga "

Zipo  changamoto  mbali mbali ambazo iwapo  atapewa  muda  wake wa kipindi japo  kimoja cha miaka 5  kuanzia mwakani 2015  tungependa atusaidie  kutatua  ni pamoja na adha  ya maji na uboreshaji wa  shule za msingi ambazo nyingi  hazipo katika hali nzuri .

Hata  hivyo mbunge  Mgimwa alisema malengo  yake ni  kuweka rekodi  nzuri ya ubunge katika  jimbo  hilo la Kalenga na kulifanya kuwa  jimbo lenye maendeleo makubwa  ikiwa ni pamoja  na kuona ndoto  yake ya kuanzisha  benki ya  wananchi wa Kalenga  inaanzishwa  ili  kusaidia  kuwakopesha  wakulima mitaji .

Kuhusu  suala la maji alisema  tayari katika baadhi ya maeneo ameanza  kutekeleza ahadi ya  maji  safi pamoja na kupeleka  umeme katika kata ya Mgama na Magulilwa ili  kuchochea kasi ya maendeleo japo  maombi  yake kwa  wananchi ni  kuendelea  kumwombea  zaidi  ili ndoto  yake ya kuleta maendeleo ifanikiwe zaidi.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.