Friday, October 31, 2014

FILIPE NYUSI ALIPATA MIKOBA YA CCM KUSHINDA UCHAGUZI MSUMBIJI

   Rais wa Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi akisoma gazeti la Uhuru wakati akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuja kwenye ziara ya siku tatu mwezi Julai mwaka huu nchini Tanzania ambapo alitembelea jiji la Dar es salaam,Tanga na Zanzibar.
   Frelimo na CCM wana urafiki mkubwa sana kiasi cha kusaidiana katika mikakati ya kupata ushindi kwenye chaguzi zao.


Kilifuatilia kwa karibu kwa kuwa pia CCM na Chama cha FRELIMO ni vyama ndugu vyenye historia moja na ya pamoja ya Ukombozi Kusini mwa Afrika.

Historia hiyo ndiyo iliyomfanya Rais Mteule wa nchi hiyo Ndugu Filipe NYUSI mara baada ya kuteuliwa kwake na FRELIMO kugombea Urais, nchi ya kwanza kuitembelea kuwa Tanzania.

Ikumbukwe kwamba huyu si mgeni hapa Tanzania. Kama wanaharakati wengine wa ukombozi, Ndugu NYUSI aliishi Tanzania, anaongea vizuri Kiswahili na anaichukulia Tanzania ni nyumbani.
Share:

Select Language

CCM Blog VIEWERS

All posts in this blog

General comments/advise

Google+ Followers

Powered by Blogger.