LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Apr 16, 2013

ZIARA YA KINANA ULANGA, MOROGORO‏

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa Magdalena Mashinga, alimkabidhi kadi za CCM kwa wanachama wapya kwenye tawi la CCM la Mawasiliano, wilayani Ulanga,Aprili 15, 2013, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama mkoani Morogoro. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib na Mwenyekiti wa CCM mkoa hu, Innocent Edward. (Picha na Bashir Nkoromo).

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Katibu wa tawi la CCM  Kiwanjani, Ulanga,mkoani Morogoro,  Francis Kanyali aliyekuwa akisoma taarifa, Kinana alipotemebea tawi hilo kukagua uhai wa Chama, Aprili 15, 2013. (Picha na Bashir Nkoromo).


Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib akikagua daftari la wanachama wa CCM kwenye tawi la Mawasiliano, Ulanga mkoani Morogoro, alipofika hapo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Aprili 15, 2013. (Picha na Bashir Nkoromo).


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akiwa katika picha ya pamoja na  viongozi wa CCM tawi la Ulanga Mjini mkoani Morogoro, baada ya kukagua uhai wa Chama kwenye tawi hilo, Aprili 15, 2013. (Picha na Bashir Nkoromo).

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Pancras Mogela aliyekuwa mwanachama wa Chadema akipoamua kujiunbga na CCM, Kinana alipotembelea tawi la CCM Viwanjani, Ulanga mkoani Morogoro, kukagua uhai wa Chama kwenye tawi hilo, Aprili 15, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib. (Picha na Bashir Nkoromo).


Kinana akipokea kadi ya mwanachama mpya kutoka Chadema, Kijiji cha Mwaya.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi Mbuzi kwa Nahodha wa timu ya Libenenga, Steven Maundu, baada ya timu hiyo kuibuka mshindi kwa kuibugiza timu ya Nkongo mabao 2-0, katika mechi ya fainali ya Kinana CUP, kwenye Uwanja wa Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Pamoja na zawadi hiyo, ameipatia timu hiyo zawadi ya sh. 100,000 kiasi kinacholingana na alichoipa timu iliyofungwa. Kulia ni  Nahodha wa timu ya Nkongo, Abdallah Mazengo. (Picha na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages