Katika mkutano wake na Waandishi wa Habari,uliofanyika leo
asubuhi Kizota mjini Dodoma,Nape alizungumzia kufanikiwa kwa siku ya jana, baada
kila kitu kwenda vizuri kwa mujibu wa ratiba.
Pia alizungumzia ratiba ya leo,ambapo kutakuwa na Taarifa
mbali mbali za kazi za chama,Taarifa za utekelezaji za ilani ya uchaguzi (Bara
na Zanzibar) itasomwa na Waziri Mkuu Mizengo Kayanda Pinda kwa upande wa
Tanzania bara na kwa upande wa Tanzania visiwani itasomwa na na Makamu wa Pili
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd.Taarifa kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pia zitasomwa leo.
Akizungumzia mabadiliko ya Katiba,alisema kumekuwa na mafanikio
sana baada ya mapendekezo yote kupitwa bila kupingwa,moja ya mapendekezo ni
kuwepo kwa Baraza la Ushauri la Wazee, pamoja kubariki mapendekezo wajumbe wa halmashauri
kuu ya Taifa watoke wilayani.
Baada ya uchaguzi kutakuwa na mrejesho wa mijadala na kutoa
maazimio ya Mkutano Mkuu.
1.hongera kwa kumweka mangula hapo.
ReplyDelete2.Nape usitetereke matunda yako yanaonekana kidogokidogo.
3.Viongozi twawaomba mshikamane kuanzia hapo mlipoanza leo hapo DODOMA.