AJALI ZA BODA BODA ZAZIDI KUONGEZEKA

Wananchi wakiangalia ajali ya pikipiki iliyotokea Barabara ya Nyerere eneo la Njia panda ya Vingunguti jana, ambapo ilielezwa kuwa dereva wa pikipiki hiyo aliumia vibaya na kukimbizwa hospitali. Haikuweza kufahamika chanzo cha ajali hiyo iliyofanya pikipiki kubondeka na kuwa kama chapati kuanzia mbele hadi tenki la mafuta na kubaki tairi la nyuma pekee.