LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 11, 2025

KUMBE RAIS ZUMA NA RAIS KIKWETE WALIPAMBANA KUMUOKOA KANALI GADDAFI ASIUAWE

No fly Zone in Libya- NATO.


Jasho jembamba lilianza mtiririka Rais Jakaya Kikwete Baada ya kupata habari rasmi kuwa hakutakuwa na ndege ya kuruka au kutua Jijini Tripoli Libya na ndege itakayokiuka itatunguliwa.

Hofu ya kumpoteza mmoja wa viongozi wakubwa Afrika tena yeye akiwa  ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), hakutaka hili litokee, hakutaka awe shahidi wa hili, hakutaka aje alaumiwe kwa kushindwa kutoa msaada kwa kiongozi mkubwa Afrika ambaye dalili za kuendelea kuishi zilikuwa zikiyeyuka kama theluji jangwani.
******
Rais Jakaya Kikwete akavuta uzi kwa swahiba wake pale kwa Madiba Mzee wa Bata Rais Jacob Zuma, vichwa viwili vikatoka na azimio moja Rais Jakaya azungumze na Barack Obama Rais wa Marekani.
****
Rais Barrack Obama alitoa kauli moja nzito, "Hakuna namna mtaweza kumsaidia Gaddafi zaidi ya Gaddafi  mwenyewe aamue kuondoka Libya." 

Obama akaulizwa, " Ataondokaje Libya na tayari NATO wameweka No fly Zone!?

Obama, "Zungumzeni nae akikubali basi ndege iliyombeba yeye na familia yake yote itaruhusiwa kuruka anga la Libya."
****
Kanali Gaddafi alikataa aliona kama mpango wa kuteketezwa yeye na familia yake yote, hakuta yatokee yale ya Saddam Hussein ambaye yeye na watoto wake Udday Na Ussay waliuawa kikatili, aliona huu ni mtego.
****
Plan yake Kanali Gaddafi ikawa kwenda zake mji alikozaliwa wa Sirte. Kule angevuka border kwenda ng'ambo. 
****
Rais Kikwete na Rais Zuma hawakuchoka wakaomba tena kibali Ndege ya Rais wa Afrika Kusini "South African Presidential Jet" itue Tripoli Libya imbebe Kanali Gaddafi na familia yake yote wakapewe Hifadhi Afrika Kusini bado Kanali Gaddafi alikataa na ndege ilirudi tupu kwa madiba.
****
Hapa  ndipo walikata tamaa na kumuacha na msimamo wake usioyumba, "Nitafia Libya".
Jr.
2025.



 

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages