Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri nchini kutumia sehemu ya mapato yao ya ndani kujenga uzio katika shule kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na rasilimali.
Ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari na za Msingi kwenye Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Desemba 12, 2024.
Naye Rais wa Chama hicho, Denis Otieno ametoa shukrani na pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuingiza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya shule nchini, pamoja na kutatua changamoto mbalimbali katika sekta hiyo ya elimu nchini.
Wajumbe wa mkutano mkuu ambao ni wakuu wa shule za sekondari na za msingi nchini wakiwa makini kumsikiliza Waziri Mkuu.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri akijadiliana jambo na Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇