Na Mwandishi wetu, Simiyu
Kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa
waajiri waliofika kwenye banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kutaka
kujua jinsi ya kujisajili na kuwasilisha madai ya fidia kupitia mtandao yaani
Online Registration System-WCF Portal (ORS), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bw.
Masha Mshomba amesema.
Bw. Mshomba ameyasema hayo Agosti
8, 2020 kwenye banda la Mfuko huo katika maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa
kwenye viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
“Imekuwa ni nafasi nzuri sana
ya mfuko kuelezea huduma zake hususan huduma mpya ambazo zinapatikana kupitia
mtandao zinaanzia katika hatua ya mwanzo kabisa ambayo mwajiri anataka
kujisajili katika mfuko, kuleta michango kupitia mtandao lakini kubwa zaidi ni
jinsi ya kutoa taarifa (kuwasilisha madai) endapo mfanyakazi amepata ajali au
ugonjwa utokanao na kazi.” Alisema Bw. Msomba.
Alisema katika maonesho hayo
waajiri wengi walifika katika banda la WCF wakiwa na shauku kubwa ya kuelewa
jinsi ya kujisajili na kuwasilisha madai kupitia mtandao.
“Tumepata mwitikio mzuri sana
karibu waajiri 200 wamefika kujisajili kupitia mtandao na hii inaonyesha ni
jinsi gani suala la matumizi ya mtandao limerahisisha sana utoaji wa huduma za
mfuko na hii inakwenda sambamba na azma nzima ya serikali yetu inayoongozwa na
Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ambaye anatamani sana kuona taasisi hizi za
serikali zikitumia huduma hizi za mtandao kwasababu anajua wazi kwamba
zinapunguza gharama na zinaleta ufanisi katika utendaji wa taasisi na taifa
zima kwa ujumla.” Alisisitiza.
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi
ni taasisi ya serikali yenye jukumu kubwa la kulipa fidia kwa mfanyakazi
aliyeumia, kuugua au kufariki kutokana na kazi na walengwa hasa ni watumishi
wote kutoka sekta ya Umma na Binafsi Tanzania bara.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto),
akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw.
Masha Mshomba kwenye maonesho ya Nanenane kitaifa kwenye viwanja vya Nyakabindi
mkoani Simiyu Agosti 8, 2020. Katikati ni Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Profesa Tadeo Satta
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank, Bw.Abdulmajid Nsekela (kushoto) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la WCF kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabidni mkoani Simiyu Agosti 8, 2020
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Masha Mshomba (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba wakiwa mbele ya banda la WCF katika maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu Agosti 8, 2020
Afisa Uhusiano Mwandamizi Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Sebera Fulgence (kulia) akiwapa elimu wanafunzi waliofika kwenye banda la Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi wakiongozwa na mwalimu wao ili kujifunza kuhusu masuala ya fidia kwa Wafanyakazi kwenye maonesho ya Nanenane viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇