Mgombea urais wa Tanzania, kupitia CCM, Dk. John Magufuli akijinadi katika mkutano wa hadhara katika Stendi ya Mbalizi, mkoani Mbeya. Dk Magufuli amesema kuwa ingekuwa amri yake leo angepigiwa kura na kushinda urais ili kesho yake aanze kazi.
Pia, akihutubia katika mkutano huo, amesema kuwa yeye binafsi anawachukia wezi, wabadhilifu wa mali za umma na mafisadi na kwamba kyama chao kinakuja, kwani CCM ikishinda atafungua mahakama ya mafisadi hao ili wahukumiwe haraka na kuswekwa gerezani. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Wananchi wakimshangilia Dk. Magufuli alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni mjini Mbalizi, mkoani Mbeya
Dk. Magufuli akihutubia wananchi katika Mji mdogo wa Mlowo, wilayani Mbozi, akiwa safarini kwenda Wilaya mpya ya Songwe, mkoani Songwe.
Ni furaha iliyoje kwa wakazi wa Mji wa Mlowo wakati wa kumlaki Dk. Magufuli
Dk. Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Mji mdogo wa Mlowo, wilayani Mbozi.
Wananchi wakimshangilia Dk. Magufuli alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni mjini Mbalizi, mkoani Mbeya
Wananchi wakimshangilia Dk. Magufuli alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni mjini Mbalizi, mkoani Mbeya
Wananchi wakimshangilia Dk. Magufuli alipokuwa akihutubia katika mkutano wa kampeni mjini Mbalizi, mkoani Mbeya
Aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini na kushindwa kwenye kura za maoni, Mchungaji Luckson Mwanjali (katikati) akimnadi Mgombea Urais wa Tanzania, kupitia CCM, Dk. John Magufuli (kushoto), na Mgombea ubunge wa jimbo hilo, Oran Njeza wakati wa mkutano wa kampeni mjini Mbalizi, mkoani Mbeya
Sehemu ya umati wa wananchi katika mkutano wa CCM, wa mgombea urais Dk. John Magufuli
Wasichana wakiangalia picha ya mgombea urais wa Tanzania, kupitia CCM, Dk. John Magufuli iliyobandikwa ukutani katika Kijiji cha Iyombelo Njia Panda, wilayani Songwe, Mkoa wa Songwe
Ni mwendo kwa kwenda mbele; Msafara wa Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM ukiwasili katika Kijiji cha Iyombelo Njia Panda Wilaya mpya ya Songwe mkoani Songwe.
Dk. Magufuli akijadiliana jambo na Mgombea ubunge wa Jimbo la Songwe, Philip Mulugo katika mkutano wa kampeni mjini Mkwajuni
Dk. Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano uliofanyika katika Mji wa Mkwajuni, Makao Makuu ya Wilaya ya Songwe
Mulugo akiwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020 aliyokabidhiwa na Dk Magufuli kwenye mkutano huo wa kampeni
Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, William Lukuvi (wa pili kushoto) na Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CCM, Mary Mwanjelwa wakiwapungia mikono wananchi wakati wa mkutano wa kampeni katika Mji wa Mkwajuni, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya , Abbas Kandoro na kushoto anayewatambulia ni Dk Magufuli
Wazee wakishangilia baada ya Dk Magufuli kuwaambia kuwa akichaguliwa ataanzisha mfuko maalumu wa kusaidia wazee kujikimu kimaisha
Msafara wa Dk. Magufuli ukilakiwa kwa furaha ulipowasili katika Mji wa Makongolosi, wilayani Chunya.
Kanga zikiwa zimetandikwa ili apite Dk. Magufuli alipowasili katika Mji wa Makongolosi, wilayani Chunya
Dk Magufuli na Mgombea ubunge Jimbo la Lupa, Victor Mwambalaswa wakiwasili kwenye mkutano wa hadhara katika Mji wa Makongolosi wilayani Chunya
Dk Magufuli akijinadi katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Makongolosi wilayani Chunya.
Wafuasi wa CCM wakishangilia kwa furaha baada ya Dk Magufuli kuwasili kwenye mkutano wa hadhara katika Mji wa Makongolosi ambapo alisema kuwa atawasaidia vijana na akina mama kwa kuwakopesha mitaji.
Dk. Magufuli akiwapungia wananchi mjini Makongolosi
Dk Magufuli akijinadi kwa wananchi katika Mji wa Matundasi ambapo aliwaambiwa watanzania kuwa akishinda uchaguzi watoto watasoma bure kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne.
Wanafunzi wakiwa wamebebana ili kumuoana Dk Magufuli katika Mji wa Matundasi wilayani Chunya
Wananchi wakishangilia kwa furaha walipomuona Dk Magufuli katika mkutano wa kampeni mjini Chunya.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇