Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akimtwisha mama ndoo ya maji baada ya kutembelea mradi wa maji wa Uzogero Manispaa ya Shinyanga, leo.
Na Evaristy Masuha, Wizara ya Maji
Utekelezaji wa miradi ya maji kwa kuwatumia watalamu wa wizara umeonesha kuwa na tija kwa kuwezesha miradi kukamilika kwa haraka na kwa bei nafuu huku ikiwa umetumia vifaa vyenye ubora unaostahili.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Maji Prof. Makame Mbalawa wakati akikagua mradi wa maji wa Mwawaza-Negezi unaotekelezwa katika Manispaa ya Shinyanga amapo amesema hatua hiyo imewezesha Wizara ya Maji kupanua miradi na hivyo kufanikisha lengo la Serikali la kumtua mama ndooo ya maji.
“Napenda kuwapongeza wataalamu wetu kwa hatua mliyofikia kwani utaratibu huu wa kutumia force account umesaidia kuokoa fedha na muda. Niwaombe muendeee kuwa na moyo huo ili tuifikie azima ya kumtua mama ndoo kichwani kwa haraka zaidi.”
Akitolea mfano mradi wa Mwawaza-Negezi unaotekelezwa katika manispaa ya Shinyanga amesema awali mradi huo ulipangwa kutekelezwa na wakandarasi kwa sh. Bilioni 2, Wizara ilipoamua kuutekeleza kwa kutumia wataalam wake, mradi huo ambao hadi sasa umefikia asilimia 95 ya utekelezaji umetumia Bilioni 1 huku ukitarajiwa kukamilika ukiwa umetumia shilingi bilioni 1.2 ambapo Wizara itakuwa imeokoa milioni mia nane.
Amesema Wizara ya Maji imejipanga kuendelea kuutumia mfumo huo ikiwa ni hatua ya kuhakikisha inawawafikishia wananchi maji kwa haraka na kwa njia rahisi.
Kwa upande wa miundombinu ya maji Mbarawa amesema serikali inatumia gharama kubwa kununua vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa miundmibnu ya maji hivyo wananchi wawe walinzi wa kwanza wa miundombinu hiyo.
Awali akizungumzia utekelezaji wa mradi huo Meneja Ufundi Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) Mhandisi Yusuf Katokola amepongeza wizara kwa kuwezesha kujengwa kwa mradi huo na kwamba utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji kwenye vijijji vya Mwawaza na Negezi ambavyo wakazi wwake wamekuwa wakisafiri umbari mrefu kutafuta maji.
Amesema changamoto ya maji kwa vijiji hivyo ni kubwa, ndiyo maana wameamua kufanya kazi muda wote kuhakikisha mradi huo mkubwa unakamilika ndani ya miezi sita huku wananchi wa vijiji vya Negezi wakiipongeza serikali na kuiomba ikamilishe mradi huo kwa haraka. Hussein John mkazi wa Mwawaza amesema wamekuwa wakikubama na changamoto nyingi ndani ya ndo zao kutokana na wanawake kuchelwa wanapokuwa wanafuatilia maji. Ujio wa mradi huo utasaidia kupunguza kero hiyo.
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko mara baada ya kutembelea mradi wa maji wa Mwawaza-Negezi
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbarawa akizungumza na wananchi. Alipotembelea mradi wa maji wa Uzogero Manispaa ya Shinyanga
Tenki la Maji la mradi wa maji wa Mwawaza-Negezi Manispaa ya Shinyanga
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇